• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Bilioni 25 kunufaisha wavuvi, Wafugaji wa samaki 2000 kanda ya ziwa:Waziri Ulega

Posted on: October 3rd, 2023

*Bilioni 25 kunufaisha wavuvi, Wafugaji wa samaki 2000 kanda ya ziwa:Waziri Ulega*


Wanufaika 2000 kutoka sekta ya Uvuvi kutoka mikoa ya Mwanza,Kagera,Mara,Geita na Simiyu watanufaika na mradi wa kisasa wa ufugaji wa samaki na Uvuvi kwa kukabidhiwa boti za kisasa na vizimba ukiwa ni mkakati wa Serikali ya awamu ya sita ya kuinua uchumi wa wananchi.

Akizungumza leo Mkoani Mwanza Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati wa ziara yake ya kukagua Boti 55 na Vizimba 273 zitakazotolewa kwa makundi mbalimbali,amesema mkakati huo ni uwezeshaji kwa wananchi kwa vitendo kwa mkopo nafuu usiyo na riba.


"Hii haijawahi kutokea ni kwa mara ya kwanza Serikali ya Rais Samia inafanya jambo hili kubwa, unakabidhiwa boti ya kisasa yenye vifaa vyote muhimu vikiwemo vya kubaini sehemu walipo samaki na mahali pa kuwahifadhia",Mhe.Ulega.

Amebainisha baadhi ya wafugaji wa samaki wa vizimba watakabidhiwa pia boti kwa ajili ya kuwasaidia safari ya kwenda eneo la mradi wao na wavuvi watakabidhiwa boti za ukubwa tofauti kulingana na ombi lao.

"Nimefarijika kuziona boti hizi na vifaa vyake,hivi karibuni Mhe.Rais amekabidhi boti za uvuvi huko mkoani Pwani kwani Serikali imetoa jumla ya boti 165 na vizimba 165  kwa wanufaika upande wa Bahari na Maziwa,"amesisitiza Waziri Ulega.

Aidha amesema fedha hizo zimetolewa na Serikali na kukabidhiwa Benki ya Kilimo ya TADB na baada ya miaka minne itaanza kupokea marejesho ya mkopo huo na umetolewa muda huo ili kuwapa nafasi wanufaika kujipanga vizuri na miradi yao.

Amewataka pia wanafukaika wote watembelee na kujionea vyombo vyao  vilivyopo maeneo ya Chuo cha Uvuvi Nyegezi kabla ya Mhe.Rais hajawakabidhi rasmi.

"Wanufaika wa mradi huu ni vikundi vya ushirika 23,Kampuni 10, na watu 28 huku Mwanza wakiwa na wanufaika 29 ambao ni wengi zaidi kulinganisha na mikoa mingine,"Nazael Mandala,Mkurugenzi  Ukuzaji Viumbe maji,Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Mradi huu utawasaidia wanafaika hao kuvuna samaki zaidi ya Tani elfu tano hadi kumi.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti