• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Brela watambulisha mfumo wa kupata reseni kwa njia ya Mtandao

Posted on: September 8th, 2019


Mamlaka ya Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELA) imetambulisha mfumo mpya wa kutuma maombi ya leseni  ya biashara kwa wadau wa biashara utakaokuwa unafanyika kwa njia ya mtandao badala ya kutumia fomu za kawaida ili kuwasaidia  kupata kibali kwa wakati.


Akizungumuza jijini Mwanza wakati wa semina elekezi kwa wadau wa biashara, Mkurugenzi wa Utawala na Fedha  kutoka Brela, Bakari Mketo alisema  mfumo huo unakuja kutatua changamoto ya mlolongo mrefu wa uombaji leseni za biashara  ambapo hivi sasa  leseni itatolewa punde tu baada ya  taarifa zitakapohakikiwa na malipo kufanyika.


“Tupo hapa kuleta elimu  ya utoaji wa leseni kwa njia ya mtandao, kama mnavyojua tulitangulia kufanya hivyo kwa upande wa makampuni, majina ya biashara, alama za biashara na leseni za viwanda na sasa Brela tumepewa jukumu jipya la utoaji wa leseni  daraja la kwanza ‘Class-A’ ambayo awali ilikuwa inatolewa na wizara ya viwanda na biashara.


“Na kwa sababu hii leseni  hii ina uhusiano mkubwa na leseni daraja la pili ya class-B zinazotolewa na halmashauri, hivyo ili kuepusha kutoa leseni tofauti kwenye nchi moja kwa wadau wetu lazima leseni hizi zitoke zikiwa zina sura moja na namna moja ya upatikanaji, hivyo zote kwa pamoja zitapatikana kwa njia ya mtandao ili kumpunguzia milolongo mirefu mteja wetu kwa maana ya gharama na muda.


“Sasa tupo kwenye hatua za awali za upandikizaji mfumo huu kwenye halmashauri sita zilizochaguliwa  ambazo ni Mwanza, Bukoba, Karagwe, Ilala, Chalinze na Mafinga kabla ya kurasimishwa nchi nzima kwani halmashauri hizi zitatoa picha kamili ya mwenendo wa mfumo huu ili kama kuna changamoto tuzifanyie kazi mapema,” alisema Mketo.


Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Joseph Kahungwa alisema kuwa mfumo ulioanzishwa na Brela ni mzuri pia ni kama neema kwa wajasiliamali wapya kwani utawapunguzia wafanyabiashara usumbufu wa kufunga safari kwenda makao makuu Dar es Salaam kufuata leseni ya biashara.


“Mimi kama mdau wa biashara nimependa mfumo huu ingawa tumewaomba wahusika kurahisisha zaidi hasa kwa kutengeneza mfumo ambao vibali vyote vitatolewa kwenye nyaraka moja itakayoambatanishwa badala ya kuwa na  nakala tofauti tofauti za vibali ili kurahisisha zaidi zoezi la kutuma maombi,”alisema Kahungwa.


Naye Afisa Biashara kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Josephine Lyimo amesema mbali ya mfumo huo kuokoa muda wa upatikanaji leseni za biashara  pia utasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza mianya ya rushwa waliyokuwa wakikutana nayo wafanyabiashara wakati wa ufuatiliaji wa leseni zao, hivyo itachagiza wajasiriamali wengi wapya kufanikisha adhima yao.


Semina hiyo iliyofanyika kwa muda wa siku tano mfululizo imewakutanisha kwa pamoja wafanyabiashara, wanasheria, wakaguzi wa mahesabu, TCCIA, pamoja na Brela wenyewe ili kuongeza uelewa zaidi wa mfumo huo mpya kwa wadau tofauti wa biashara na kuondoa ugeni wa mfumo huu kwa watanzania wote kwa ujumla.







Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti