• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Butimba Yakabidhiwa zawadi ya ushindi

Posted on: September 2nd, 2019


Shule ya Msingi Butimba  ‘B’ imeibuka mshindi wa kwanza  katika mtihani maalum uliotungwa na Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na  maafisa elimu wa Jiji la Mwanza na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ambapo imekabidhiwa zawadi.

Mtihani huo ulifanyika wiki iliyopita kwa kushirikisha shule nne bora  kutoka Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela ambazo ni Butimba A na B, Bwiru na Gedeli ambapo  matokeo yametangazwa  na Afisa Elimu Mkoa, Michael Ligola ambapo alisema  lengo ni kutaka kuona shule za  kutoka Mwanza zinaingia katika orodha ya shule 10 bora kitaifa katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba unaotarajiwa kuanyika Septemba 11 na 12, mwaka huu.

Ligola amesema  wanafunzi wa Shule ya  Msingi Butimba ‘B’ wamefaulu kwa zaidi ya asilimia 100  katika masomo yote, mshindi wa pili ni Butimba A, mshindi wa tatu ni Bwiru na Gedeli imekuwa ya mwisho  ambapo amebainisha somo ambalo limeonekana kutokuwa na matokeo mazuri ni Kiswahili.

Ligola alisema kutokana na matokeo hayo yamempa imani shule za Mwanza zitaingia katika orodha ya shule 10 bora kitaifa katika mtihani unaotarajiwa kufanyika huku  akitangaza  kwamba kuanzia sasa wanafunzi wataweka kambi mashuleni kwa lengo la kuhakikisha kasoro zilizojitokeza zinaondolewa.

Akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wanne, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Christopher Kadio, amesema hakuna sababu inayozuia shule za Mwanza kuingia katika orodha ya shule 10 kitaifa kwa kuwa kila rasilimali zipo, hivyo aliwataka wanafunzi kuongeza juhudi na  siyo kubweteka na matokeo hayo.

“Mwanza tunatakiwa kufanya vizuri  katika mtihani kwa sababu kila rasilimali zipo na nimedokezwa kwamba mtihani mliofanya umetungwa kwa mfumo wa mtihani wa taifa ambao mnatarajia kuufanya Septemba 11 na 12 mwaka huu, hivyo naomba muongeze bidii zaidi kwa siku zilizobaki.

“Hapa mshindi wa kwanza  tutamkabidhi mbuzi mmoja tena beberu na fedha taslimu ambazo mtatumia katika kufanikisha mahafali yenu baada ya mtihani wa taifa, mshindi wa pili, wa tatu na wanne tutawapa fedha taslimu  lakini kikubwa nawaomba muongeze jitihada, tunataka shule 10 bora na Mwanza iwemo,”alisema.

Hata hivyo  Kadio alitoa Sh. 20,000 kwa   kila mwanafunzi, kwa wale 10 waliofanya vizuri katika mtihani huo.Pia aliwaahidi walimu wakuu wa Shule za Butimba, Bwiru na Gedeli  kwamba changamoto zilizopo katika shule hizo zitafanyiwa kazi haraka ili kusiwepo na kisingizio tena.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Butimba, Dotto Emmanuel alisema shule hiyo kufanya vizuri ni desturi yao na kuahidi kwamba atawashangaza watu  kuingia 10 bora kitaifa ingawa haijawahi kutokea.Hafla hiyo imehudhuriwa na maafisa elimu jiji la Mwanza,  Manispaa ya Ilemela baadhi ya walimu na wanafunzi.

Hivi  karibuni Serikali mkoani Mwanza iliweka  maazimio 14 kwa walimu wakuu, maafisa  elimu wa kata na taaluma ili kuinua ufaulu kwa shule za msingi 2019/2020 ambapo mitihani hiyo ni sehemu ya utekelezaji  kwa vitendo kwa wanafunzi wa darasa la saba wanaotarajia kufanya mtihani wa taifa kati ya Septemba 11-12, mwaka huu.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti