• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Elimu ya Afya yatolewa Mwanza

Posted on: May 8th, 2021

Wito umetolewa kwa watu wenye tatizo la shinikizo la damu kufanya mazoezi na kuepuka ulaji usiopangiliwa huku tahadahari ikitolewa kwa wanaojikita kutumia tiba asili ambazo hazijafanyiwa utafiti.

Wito huo umetolewa na Daktari bingwa mbobezi wa magonjwa ya figo na shinikizo la damu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Ladislaus Rudovick,wakati hospitali hiyo ikiadhimisha siku ya Shinikizo la Damu Duniani kwa kutoa huduma za upimaji afya bure kwa magonjwa yasiyoambukiza.

Dkt.Rudovick alisema,suluhisho la kwanza kwa mtu mwenye tatizo la shinikizo la damu ni kufanya mazoezi na kuepuka ulaji usiopangiliwa.


Huku akitoa tahadhari kwa wale wanaojikita zaidi kwenye tiba asili ambazo hazijafanyiwa utafiti kwani moja ya  changamoto ni kupata madhara mengine yanayoweza kusababisha matatizo zaidi ya kiafya, ikiwemo kuharibu figo.


Akizungumzia ugonjwa wa shinikizo la damu Dkt.Rudovick, alisema ugonjwa huo umegawanyika katika sehemu kuu mbili ambapo ya msingi hubainika zaidi kwa wale wenye umri wa kati ya miaka 30 hadi 50 na chanzo chake kwa asilimia 90 hadi 95 huwa hakijulikani.

Huku ya sekondari ni chini ya umri wa miaka 30 au zaidi ya miaka 55 ambayo chanzo chake hujulikana na wakiondoa chanzo basi tatizo linakwisha jumla.

Alisema,baadhi ya  visababishi  ni pamoja na mishipa ya kwenye figo kuwa miembamba, uvimbe tumboni na matatizo ya tezi yanayopelea homoni mwilini kuongezeka pamoja na mfumo wa maisha ambao  unaweza kuwa chanzo kikubwa hasa kwa watu wenye kipato kizuri kinachopelekea ulaji usiopangiliwa pamoja na kukosa muda wa kufanya aina yoyote ya mazoezi.


“Utakuta mtu anatoka ndani kwake na kuingia kwenye gari hadi ofisini huku muda wa kazi ukiisha anaingia tena kwenye gari, anapita sehemu za burudani, anaagiza nyama, tena ile nyekundu na kileo, hasa bia, kisha anarudi nyumbani anaoga na kulala, na kesho yake hivyo hivyo,”alisema.


Kwa upande wake  Daktari Nelly Mwageni,alisema magonjwa ya ngozi  nayo pia huendana na umri wa mtu ambapo  watoto chini ya umri wa miaka 12 wao husumbuliwa zaidi na pumu ya ngozi ambayo chanzo chake mara nyingi ni kurithi kutoka katika ukoo na baadhi ya dalili ni kuwashwa macho na mafua ya mara kwa mara.


“Mara nyingi hujitokeza kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa,mwingine mvua nyingi au joto kali ni tatizo na mwingine msimu wa mazao kutoa maua ni shida,mfano ule ungaunga unaotoa maua ya mahindi ukimpata mtoto wa tatizo hilo anaathirika,” alisema.


Ambapo vijana mara nyingi hupatwa na tatizo la mba na chunusi kutokana na balehe, wazee ni ngozi kuwa kavu kutokana na upungufu wa uwezo wa mwili kuzalisha mafuta.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti