• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Elimu ya maadili yatolewa Mwanza kwa Viongozi

Posted on: December 10th, 2020

Viongozi wa Serikali na wadau mbalimbali watakiwa kuishi kwa maadili na uadilifu ili kujenga nguzo bora yenye  kuleta tija katika kukuza na kuchochea maendeleo ya nchi.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella alipokuwa  Akifungua kikao kazi cha maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu iliyofanyika Jijini Mwanza, amesema kufuata maadili siyo matukio bali inapaswa kufanywa kwa maisha ya kila siku .

" Mfano mtu anakunywa hakatazwi lakini kuna sehemu kiongozi kama Mkuu wa Mkoa hupaswi kuwa zaidi ya masaa mawili lakini unakuta mtu anakunywa mpaka anashindana kuzungusha laundi ukiulizwa unasema nalinda kura au naamasisha wananchi huku ndipo wapo wengi tuache tabia hizo na tujidhibiti na kufanya Kazi ipasavyo kama anavyofanya Rais Magufuli ili kuleta maendeleo kwa kasi" amesema Mongella.

Naye Katibu Msaidizi wa maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Ziwa Godson Kweka akiwasilisha mada ya maadili amesema  madhara ambayo yanawezwa kuletwa na kiongozi asiyekuwa na maadali ni makubwa hivyo yawapasa kutambua uongozi ni dhamana ya kuhakikisha unatekeleza majukumu uliopatiwa kikamilifu.

" Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Uzingatiaji wa ahadi ya uadilifu kwa viongozi na watumishi wa ustawi wa utawala bora na haki za binadamu", watumishi mtambue nafasi mlizopewa ni kwa maslahi ya umma na kuwatumikia wananchi na kutotumia nafasi hiyo kwenda kinyume na maadali wengine wanatumia nafasi zao vibaya kwa kutowajibika,kujihusisha, kuwanufaisha marafiki, ndugu na siyo jamii " amesema Kweka.

Naye Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza Emmanuel Stenga akiwasilisha hali ya rushwa kwa mkoa amesema wamekuwa wakitekeleza majukumu ya kisheria ya kuzuia ,kuelimisha na kupambana na rushwa na kutekeleza maagizo ya Rais Magufuli ya kutetea wanyonge dhidi ya vitendo vya dhuluma na visivyo vya kiutu.

Ameongeza kwa kipindi cha Julai 2015 Hadi Juni  2020 kwa dawati la uchunguzi pekee TAKUKURU Mkoa wa Mwanza imekamilisha uchunguzi wa majalada 209,kesi 125 zimefikishwa mahakamani, kesi 62 washtakiwa wametiwa hatiani, kesi 49 washtakiwa wameachiwa huku majalada 30 ya watumishi yaliyokuwa yakichunguzwa wamechukuliwa hatua za kinidhamu.

"Kwa kipindi cha mwaka mmoja wa fedha uliopita,Julai 2019 hadi Juni 2020 TAKUKURU mkoani hapa imepokea taarifa 831 , taarifa hizi zinahusisha makosa ya rushwa,makosa mengine ya jinai ambayo siyo rushwa ,vitendo vya dhuluma, ucheleweshaji ama kunyimwa huduma na haki" anaeleza Stenga.

Kwa upande wake Afisa Mfawidhi Afisi ya Kanda ya Mwanza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora Albert Kakengi amesema dhana ya utawala bora ni pana ambayo inasisitizwa duniani kote kuwa ndiyo msingi utaofikia malengo ya milenia, pia ukuaji wa uchumi utasaidia kupunguza umaskini wa kipato na kuimarisha ubora wa maisha na ustawi wa Jamii na isipozingatiwa itachukua muda mrefu kuyafanya hayo.

Dkt.Jacob Mutash ambaye ni Mchungaji wa kanisa la EAGT Kiloleli na Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeki akizungumzia suala la maadili na uadilifu walisema viongozi wanapaswa kuwa na hofu ya Mungu na kuyazingatia kwa kutenda yale yaliomema na kuwa na bidii ya kutenda kazi ili kuijenga nchi yenye kuleta nuru kwa watu wote.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti