• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Fursa za Uwekezaji Mwanza Zaivutia Korea ya Kusini

Posted on: February 27th, 2018


Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza imepokea wageni kutoka Korea ya Kusini wakiwakilisha Kampuni za uwekezaji zilizopo Nchini humo kwa ajili ya kutafuta fursa za uwekezaji Mkoani Mwanza baada ya kutembelea Tovuti ya Mkoa na kusoma Mwongozo wa Uwekezaji.

Akiwatambulisha wageni hao, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Wazawa yenye makazi yake Zanzibar ijulikanayo kama Drums of Africa Limited  Bwana Harun B. Mohamed ambaye ni mwenyeji wao amesema, Kampuni yake imepokea  wageni hao wakiwa ni Kampuni mbili tofauti (U & I  International) na (EK Engineering) na wana nia na uwezo wa kutaka kuwekeza Mkoani hapa.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amewakaribisha wawekezaji hao na kuwaambia kuwa Mkoa umejipanga kuhakikisha kwamba unafanikisha sera ya viwanda na kuifanya Tanzania kuwa ni Nchi  ya uchumi wa kati  kwa kuweka mazingira wezeshi  kwa wawekezaji.

“Kwa kuwa mmeonyesha nia ya kuwekeza Mwanza sisi tumefarijika na tupo tayari kuwapa ushirikiano wa hali ya juu kulingana na maeneo mtakayotaka kuwekeza” alisema Mongella.

Aidha, Mhe. Mongella amewataka wawekezaji wote wa ndani na nje kufika Mwanza kuona fursa na kuwekeza kwa kuwa uwekezaji Mwanza unatija kubwa kwa mwekezaji kwani Mkoa umejipanga, pia ni sehemu inayofikia kwa urahisi zaidi.

Naye, Bwana John Kim akiwakilisha Kampuni ya U & I International amesema amefarijika sana na mapokezi kwani ni mara ya kwanza kufika Mkoani hapa, hivyo wanakwenda kupitia mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mwanza waone ni sehemu gani wanaweza kuwekeza.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti