• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

FURSA ZA UWEKEZAJI MWANZA ZIPO ZA KUTOSHA KUANZIA VIWANDA, MADINI, UVUVI NA UTALII: RAS MWANZA

Posted on: August 15th, 2024

FURSA ZA UWEKEZAJI MWANZA ZIPO ZA KUTOSHA KUANZIA VIWANDA, MADINI, UVUVI NA UTALII: RAS MWANZA


Timu ya wafanyakazi kutoka Ofisi ya Gavana Jimbo la Jiangsu nchini China leo Agosti 15, 2024 imefanya mazungumzo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza aliyewakilishwa na Bw. Daniel Machunda ambaye ni Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu lengo likiwa ni kuimarisha uhusiano na jiji la Mwanza katika nyanja mbalimbali.

Akizungumza na wafanyajazi hao Machunda amesema uhusiano huo utakuwa na tija kwa pande hizo hasa kutokana na Mkoa wa Mwanza kuzidi kuimarika kiuchumi na kuwepo eneo la kimkakati huku China ikizidi kupaa kwa teknolojia  Duniani.

Aidha, Machunda amebainisha kuwa Gavana wa Jimbo hilo Mhe. Xu Kunlin anayetarajiwa kuja mwishoni mwa mwaka huu atavutiwa na fursa nyingi atakazoshuhudia mkoani humo kama za Viwanda, Madini, Ufugaji, Uvuvi pamoja na Utalii.

"Ndugu zangu wageni Mkoa wa Mwanza una idadi kubwa ya Mifugo na pia sehemu kubwa ya ziwa Victoria ipo Tanzania hivyo unapotaka kuwekeza kwa upande wa usindikaji wa nyama au ngozi au Ufugaji wa kisasa wa samaki Mwanza ni eneo mwafaka kabisa", amesema Machunda wakati akitoa taarifa fupi ya Mkoa huo kwa  wageni hao kutoka Jimbo la Jiangsu.

Ameongeza kuwa Tanzania na China ni Mataifa ndugu na marafiki kwa miaka mingi , uhusiano ambao uliasisiwa na viongozi wa zamani wa nchi hizi Hayati Julius Nyerere na Mao Tsetung na kufanya raia wa pande hizo mbili kuzidi kufaidika kwenye sekta mbalimbali.

Akizungumzia ziara ya wageni hao Mkuu wa Idara ya viwanda, biashara na uwekezaji Patrick Karangwa amesema Mkoa wa Mwanza unazidi kupata umaarufu kutokana na mvuto wake wa kuwekeza hivyo wageni hao wamepata wigo mpana kabla ya kufika rasmi Gavana kutoka jimboni kwao.

"Kama alivyotangulia kusema Kaimu Katibu Tawala, wageni hawa watapata fursa ya kujionea miradi mbalimbali inayokwenda kuimarisha uchumi wa mkoa huu na kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji, huu ni mwanzo mzuri wa safari ya uwekezaji". Karangwa.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti