• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

HISTORIA YAANDIKWA DARAJA LA J.P MAGUFULI LAFUNGULIWA RASMI

Posted on: June 19th, 2025

HISTORIA YAANDIKWA DARAJA LA J.P MAGUFULI LAFUNGULIWA RASMI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo juni 19, 2025 amezindua na kufungua rasmi daraja la J.P Magufuli lenye urefu wa Kilomita tatu lililojengwa na kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporationi (CCECC) kwa gharama ya Shilingi bilioni 718 pamoja na VAT.

Akizungumza na wananchi katika hafla ya ufunguzi iliyofanyika katika viwanja vya chuo cha ufundi Kalwande wilayani Misungwi Mhe. Rais amesema serikali imejidhatiti katika kuwaletea wananchi uhakika wa usafiri na usafirishaji na ndio maana kwa nyakati tofauti imeendelea kuboresha vivuko na hatimaye ujenzi wa daraja.

Dkt. Samia amesema, tangu aingie madarakani amehakikisha anakamilisha ndoto za hayati Rais wa awamubya tano ikiwemo kukamilisha miradi ya kimkakati ukiwemo daraja hilo na kwamba anayo furaha kufuta historia zenye huzuni za usafiri duni za wananchi kutumia muda mrefu kuvuka upande mmoja hadi mwingine na kwa sasa watu watatumia dakika 4 tu.

Aidha ametoa wito kwa jamii, wizara ya Ujenzi pamoja na vyombo vya ulinzi kulilinda daraja hilo na akawasihi wananchi kuongeza uzalishaji kwenye kilimo, ufugaji na biashara ili kuongeza tija kwenye maisha yao kwani daraja litaleta fursa ya kuimarisha biashara ya kikanda baina ya Tanzania na nchi za jirani.


Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) amemshukuru Mhe. Rais kwa kuandika historia ya upendo kwa kuendeleza ujenzi wa daraja la JP Magufuli kutoka asilimia 25 hadi 100 ikiwa ni kwa kulipa zaidi ya bilioni 450 akiwa amekuta yamefanyika malipo ya bilioni 250 tu.

Amesema kuwa daraja hilo ni alama kwa taifa na kwamba kanda ya ziwa inakwenda kuchechemka kiuchumi kwa makundi yote ya wafanya biashara na wajasiriamali kwani linafunganishwa na huduma zingine za uchukuzi kutoka mradi wa SGR kupitia kituo cha Fella kilichopo Kilomita 15 tu kutoka darajani.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amemshukuru na Mhe. Rais kwa kuipatia Mwanza zaidi ya Trilioni 5.6 za miradi ya maendeleo (minne 4) na akabainisha kuwa daraja hilo litaongeza mchango wa Mkoa wa Mwanza kwenye pato la Taifa ambapo kwa sasa unachangia zaidi ya Trilioni 7 ambazo ni asilimia 7.2.

Aidha, amefafanua kuwa vivuko vilivyokua vikitumika kuvusha vitahamishiwa sehemu zingine kwa ajili ya kuimarisha huduma mathalani MV Misungwi kitapelekwa Kisorya na Rugezi na MV Sengerema kitawavusha wananchi wa visiwa vya Kanyala- Kasarazi wilayani Sengerema.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti