• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Hospitali ya Bugando wazindua huduma ya upasuaji kwa njia ya matundu

Posted on: July 15th, 2022


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel amewapongeza Viongozi na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando kwa kutoa huduma bora na za kisasa kwa wananchi wa kanda ya ziwa ambazo zimekua zikiboreshwa siku hadi siku.

Mhe. Mkuu wa Mkoa amebainisha hayo mapema leo julai 15, 2022 wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma ya Kisasa ya Upasuaji kupitia Matundu Madogo (Minimally Invasive Surgeries) katika Hospitali ya rufaa ya Kanda Bugando.

Amesema, wananchi wa kanda ya ziwa wapotao takribani milioni 14 hivi sasa wanapata huduma bora na za kisasa kabisa katika hospitali hiyo huku akizitaja huzuma za magonjwa ya Uzazi Na vizazi, njia ya mfumo wa mkojo, ubongo na upasuaji wa jumla na ametoa wito kwao kuendelea kushirikiana na Serikali na wataalamu wengine kila inapohitajika katika kuendelea kuboresha huduma.

Prof Lawrence Museru, Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili amesema kuwa nia ya Serikali kuleta huduma za kibingwa nchini tena katika sehemu  ni kuwasaidia wananchi kupata huduma hizo ndani ukizingatia wananchi wengi hawana uwezo wa kifedha kwenda kupata matibabu nje ya nchi na kwamba kwa kutumia wataalmu wa ndani kupeana mafunzo haya inasaidia Madaktari kueneza huduma za kibobezi nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt Fabian Masaga ameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya MOI kwa kuwasaidia madaktari wa Bugando kwa kuwajengea Uwezo na kufanya hospitali hiyo hivi sasa kufanya upasuaji kwa kutumia matundu madogo ambao ni wa kisasa.

"Mhe. Mkuu wa Mkoa, mpaka leo hii zaidi ya wagonjwa 18 wamefanyiwa upasuaji kwa njia ya kutumia matundu madogo kwa kushirikiana na Madaktari na wauguzi kutoka  Muhimbili na MOI na kwamba Idara zaidi ya tano tutakua tunatoa huduma za upasuaji kwa njia ya matundu madogo katika Hospitali yetu. Dkt Fabian Massaga

"Kabla ya huduma hizi ilikua mtu akipata ajali matibabu daktari alihitaji kufungua kidonda ili kufanya matibabu kama kwenye Magoti lakini sasa daktari anaingia kwenye sehemu za ndani za maungio na kuona tatizo kwa ndani na kulitibu kwa haraka na kwa njia salama kabisa. Dkt. Wilson Masanja.

"Upasuaji huu wa kisasa ni mzuri sana na hii teknolojia inamuacha mgonjwa na makovu madogo sana na hiyo inapunguza mtu kupata athari za maambukizi na unaweza ukafanyiwa leo na kesho ukaendelea na kazi zako kama kawaida" Dkt George Kanani


Awali Dkt. Samweli Byabato, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa jumla alitumia wasaa huo kuwakaribisha wananchi wa kanda ya ziwa kufanya upasuaji wa kisasa kwa kutumia matundu madogo huku akibainisha kuwa kwa upasuaji mathalani wa tumbo kifaa maalumu kuingizwa kutibu na kuondoa uchafu na mgonjwa analala siku chache na akitoka anaendelea na shughuli zake zake za kiuchumi.

"Nashukuru sana Serikali kwani mie nimefanyiwa upasuaji kwa njia hii na sijasikia maumivu sana na nimeendelea na kazi zangu hata kabla ya wiki, huduma hii ni nzuri sana maana hapo nyuma niliambiwa upasuaji ni wa hatari na unakuacha na maumivu makubwa sana." amesema Bi. Asha Bakari mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji kwa njia ya matundu  Bugando Hospitali.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti