• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

KERO YA MAJI MWANZA SASA KUTOWEKA KABISA: RC MAKALLA

Posted on: January 8th, 2024

KERO YA MAJI MWANZA SASA KUTOWEKA KABISA: RC MAKALLA


*Ampongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi za Miradi ya maji*


*Asema mikakati ipo Mwanza kuwa ya kwanza  kuchangia pato la Taifa*


*Miradi yote ya kimkakati ipo mbioni kukamilika na kuzidi kuipaisha Mwanza kiuchumi*


*Ndege ya kubeba Minofu ya Samaki kuanza kutoa huduma hivi karibuni*


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla leo Januari 8, 2024 ameipokea Kamati ya kudumu ya Bunge ya bajeti na katika mazungumzo yake amesema kero ya muda mrefu ndani ya Mkoa wa Mwanza sasa kutoweka baada ya kukamilika mradi mkubwa wa chanzo cha maji cha Butimba.


Akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Daniel Sillo kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Makalla amebainisha mradi huo wa Butimba wenye mitambo ya kisasa ambao upo asilimia 100 kukamilika utatoa kwa siku lita milioni 148 kwa siku.

"Mhe. Mwenyekiti wa kamati Mkoa wa Mwanza mradi huu sasa utawanufaisha wakazi wa Nyamagana, Ilemela, Misungwi na Magu, tunaipongeza sana kamati yako kwa usimamizi mzuri wa fedha hizi za bajeti zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya maendeleo ya wananchi," CPA. Makalla


Akizungumzia kwa ufupi miradi ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa Mkoani humo, Mkuu huyo wa Mkoa amesema ukarabati wa uwanja wa ndege utaanza Februari mwaka huu na kukamilika Juni na mizigo ya minofu ya samaki itaanza kusafirishwa kutoka uwanja huo kuanzia  Machi mwaka huu badala ya kuanzia uwanja wa Entebe na Nairobi.

"Tayari tumefanya mazungumzo na uongozi wa ATCL kuhusiana na usafirishaji wa mizigo hiyo baada ya kupata usumbufu wa kwenda kuisafirisha mbali na uwanja huu wetu wa Mwanza," amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge Mhe. Daniel Sillo amesema kamati yake imefika Mwanza ikiwa ni sehemu ya majukumu yake ya kukagua miradi yote inayotekelezwa kwa fedha za Serikali ili iweze kujionea maendeleo  na changamoto zake na baadaye kutoka ushauri kwa Serikali.

"Tuna kazi ya kuhakikisha mipango yote ya maendeleo ya kiuchumi hapa nchini inatekelezeka kama ilivyokusudiwa tupo Mwanza kukagua mradi wa chanzo cha maji Butimba, Rais wetu amekuwa mstari wa mbele kutafuta fedha na kuzitoa kwa maendeleo ya wananchi hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tuna muunga mkono kwa kusimamia ipasavyo,"Mhe. Sillo.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti