• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Workshop to complete the recruitment of new employees held in Mwanza

Posted on: September 28th, 2018


Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  kwa kushirikiana Taasisi ya Benjamini Mkapa na  Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kupitia mradi wa Mfuko wa dunia wa kupambana na magonjwa ya Kifua kikuu,Malaria, na HIV/AIDS(GFATM)na mradi wa Mkapa Fellows Program awamu ya tatu,imeendesha kikao kazi cha kukamilisha mchakato wa ajira na kuwapangia vituo vya kazi wataalamu mbalimbali wa kada za afya ambao wanatakiwa kuripoti katika  vya kazi kuanzia Septemba 25, 2018.

Akiongea katika kikao hicho cha watumishi wa ajira mpya kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  Bwana  David M. Mnkhally  Afisa kutoka Taasisi ya Benjamini Mkapa amesema orodha ya majina ya watumishi wote waliopangiwa vituo vya kazi yanapatikana kupitia tovuti ya OR- TAMISEMI ambayo ni www.tamisemi.go.tz pia katika tovuti yaTaasisi ya Benjamini Mkapa ambayo ni www.mkapafoundation.or.tz.

Mradi huu wa RSSH unatekelezwa katika Mikoa kumi ya Tanzania bara, Mikoa hiyo inajumuisha Mwanza,Shinyanga,Mara,Simiyu,Geita,Kagera,Tabora,Katavi,Kigoma na Dodoma.Ambapo jumla ya watumishi 281 wataajiriwa katika Halmashauri mbalimbali katika Mikoa tajwa hapo juu,kwa Mkoa wa Mwanza jumla ni 23, kupitia mradi wa RSSH 19 na MFP III  ni 4.

Naye  Miyeye Yahya ambaye ni Afisa kutoka Taasisi ya Mkapa ameongeza kuwa ajira hizi ni za mkataba wa mwaka mmoja na zinasimamiwa na Taasisi ya Benjamini Mkapa hivyo basi watumishi wote waliopata fursa hii watapata kipaumbele cha kujiunga na utumishi wa Umma baada ya kukamilika kipindi cha mkataba,kulingana na upatikanaji wa ajira.


Aidha Bwana Deogratias Kayombo ambaye ni Afisa Utumishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto (Afya) amesema kila mtumishi ahakikishe anazingatia misingi ya uwajibikaji na kukidhi maadili ya utumishi wa Umma katika utoaji wa huduma kwa Jamii.

Hata hivyo, Bi Hawa Waziri ambaye ni Afisa Utumishi Wizara ya Afya amesisitiza utii wa sheria katika Masuala kazi na nidhamu  ambapo amewataka watumishi kufanya kazi kwa weredi bila kubagua mtu yeyote katika kutimiza wajibu wao.

"Hakikisheni mnatimiza wajibu wenu na kuukamilisha kwa muda uliopangwa na kwa weredi,haitakiwi kutoa huduma kwa upendeleo fulani ikiwa ni pamoja na ushawishi wa kisiasa au kidini,"alisema Hawa.


Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti