• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE ATOA MAAGIZO UKAMILISHAJI DARAJA LA NGUDAMA MISUNGWI

Posted on: October 10th, 2024

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE ATOA MAAGIZO UKAMILISHAJI DARAJA LA NGUDAMA MISUNGWI


Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ndg. Godfrey Eliakim Mnzava amemuagiza Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza kuandika barua kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) na Katibu Mkuu Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili kuharakisha upatikanaji wa fedha za kukamilisha ujenzi wa daraja la Ngudama wilayani Misungwi.

Ametoa agizo hilo leo alhamisi tarehe 10 Oktoba, 2024 wakati akikagua daraja hilo linalounganisha wananchi wa vijiji vya Ngudama na Kaluluma kwa thamani ya zaidi ya Milioni 122 kutoka chanzo cha mfuko wa jimbo ambacho kinasimamiwa na Wizara hiyo.

Kiongozi huyo amesema, Mkandarasi (Barizi investiment Tanzania Limited) ameshatekeleza kazi kubwa (88%) tofauti na fedha alizolipwa jambo linalomkwamisha kuendelea na kuchelewesha lengo la serikali kuwaunganisha wananchi wa vijiji hivyo ambao kwa muda mrefu wamekua wakipata adha ya usafiri na usafirishaji wa mazao.

Aidha, amewataka TARURA Mkoani humo  kumsimamia kwa karibu mkandarasi huyo kwa kushirikiana na makao makuu yao ili kuhakikisha mkandarasi huyo anapata fedha haraka iwezekanavyo na kuweza kukamilisha ujenzi wa daraja hilo kwani ukianza msimu wa masika mvua zitamkwamisha kuendelea.

Mwenge wa uhuru wilayani Misungwi umeweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa madarasa 5 na matundu 10 vya vyoo katika shule ya sekondari Mwasonge vilivyojengwa kwa milioni 85 na kuagiza ukamilishaji wa miundombinu iliyobaki  ifikapo januari 2025 ili wanafunzi waanze kusoma hapo kwani itawapunguzia umbali wa kilomita 20 kufuata elimu.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti