• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Kwimba kusajili wanafunzi kidato cha kwanza9226

Posted on: January 4th, 2023


Mradi wa Ujenzi wa Madarasa kwa ajili ya mapokezi ya Wanafunzi wa kidato cha kwanza 2023 (Pochi la Mama) wafanikisha kuchaguliwa watoto 9226 kwa wakati mmoja kujiunga na kidato cha kwanza mapema juma lijalo wilayani Kwimba Mkoani Mwanza kutokana na Ujenzi wa madarasa 112 kwa Bilioni 2 na Milioni 240.

Akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa ukamilishaji wa Madarasa hayo uliofanyika katika Shule ya Sekondari Nyamilama ambapo yamejengwa Madarasa 12 kwa Milioni 240,  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima amewapongeza Viongozi wa wilaya hiyo kwa ushirikiano uliofanikisha zoezi hilo muhimu kwa maendeleo ya elimu nchini.

"Najua mafanikio ya Ujenzi huu ni ishara ya kuwa kila mmoja amefanya wajibu wake maana madarasa 112 sio mchezo mdogo kwani mama Samia kuleta fedha nyingi ni jambo moja lakini kutekeleza kilichoagizwa ni suala lingine na kwakweli nawapongeza wote kwa kuhakikisha jambo hili linafanikisha." Amesisitiza Mhe. Malima.

Aidha, ametoa rai kwa wanafunzi kuhakikisha wanaweka bidii kwenye Elimu ili uboreshaji wa Miundombinu na samani kwenye shule za Sekondari uendane na ukuzaji wa ufauli hasa kwa masomo ya Sayansi na amebainisha kuwa wanafunzi wanaosoma mjini wako sawa na wanaosoma shule za vijijini hivyo wasijione wanyonge.

Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi ametumia wasaa huo kuwapongeza Viongozi na wananchi wote walioshiriki kufanikisha Ujenzi na amebainisha kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kufanikisha uboreshaji wa huduma za kijamii wilayani humo kwani amepeleka fedha nyingi kwenye Sekta za Maji, Barabara na Afya.

"Rais Samia wakati anaingia madarakani alikuta wilaya hii haina umeme kwenye vijiji vyote lakini kwenye uongozi wake tumepata umeme kwenye Vijiji vyote na alikuta bajeti ya Ujenzi wa Barabara vijijini ilikua Milioni 700 lakini hivi sasa tumefikia Bilioni 3.6, ndio maana wanakwimba tunampenda." Mhe. Mageni Kasalari Mbunge wa Sumve, kwa niaba ya Mbunge wa Kwimba.

Akitoa taarifa ya Ujenzi GB wa vyumba vya Madarasa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Happiness Msanga mesema mwezi Oktoba 2022 walipokea Shilingi Bilioni 2.24 kujenga Madarasa 112 kwenye shule za Sekondari 33 na kwamba tayari Ujenzi umekamilika na wanafunzi wapatao 9226 watasajiriwa kujiunga kidato cha kwanza 2023 kwa wakati mmoja.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti