• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Kwimba Yahitaji Msukumo wa Maendeleo

Posted on: August 16th, 2018

MKuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi Ngaga kuendeleza kazi zilizokuwa zinafanywa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Mtemi Msafiri ikiwemo kukomesha  mauaji ya kishirikina, kupambana na wauzaji na watengenezaji wa  pombe  haramu (gongo) na kuzuia uharibifu wa kukata miti na kuchoma mkaa bila kufuata taratibu.

Mhe.Mongella ameyasema hayo leo Agosti 16 mara baada ya kumuapisha Mkuu wa Wilaya ya kwimba Mhe.Senyi Simon Ngaga katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

"Uende kuitafsiri nafasi uliyopewa na Mhe. Rais Dkt.John Magufuli kaendeleze vita dhidi ya mauaji ya kishirikina japo yamepungua ikiwezekana yaishe kabisa," alisema Mongella.

Mhe.Mongella aliongeza kuwa Kwimba ndiyo wilaya ya mwisho kimaendeleo Mkoani Mwanza kati ya Wilaya saba hivyo anahitaji aone mabadiliko ya kimaendeleo katika Wilaya ya hoyo.

Naye Mkuu wa Wilaya hiyo   Mhe.Ngaga ameomba  ushirikiano kutoka kwa watumishi na wana mwanza kwa ujumla ili afanikishe malengo  ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Hata hivyo alikabidhiwa vitendea kazi ambavyo ni  Katiba ya Jamuhuri ya vya Muungano wa Tanzania 1977,ilani ya uchaguzi wa Mwaka 2005,Sheria za Mitaa ya Mwaka 1977 pamoja na Masharti ya Mkuu wa wilaya ya Mwaka2016.

Awali Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Mhe. Sam Rumanyika amesema anahitaji ushirikiano katika mahama kwa wananchi na watumiahi wote kwani wanaapa kuwa waadilifu.

 "Viapo vikifuatwa mnakuwa watumishi wazuri,kwani ni uadilifu mkubwa, tumekusudia kuondoa kesi za muda mrefu na pia tumezindua kampeni katika Mkoa wa Geita,Mara na Mwanza ambao una misingi mnne itakayotusaidia katika Mahakama na wateja wetu,"alisema Mhe.Rumanyika.

"Haki yako Wajibu wangu, Napenda kesi nachukia Mrundikano, Kila mtu atende wajibu wake na Mrundikano wa Kesi ni Sumu ya Nchi"alisema Mhe. Rumanyika.

Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Mnec )wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Jamal  Abdul Babu alisema kila mtu anastahili kutii Mamlaka iliyopo madarakani na utelekezaji wa ilani utasaidia watu wachape kazi.

Aidha Mhe.Mongella alisisitiza  ukusanyaji wa mapato,utumiaji mzuri wa ardhi,kuwe na siasa safi, uongozi bora na kuwe na mkakati wa kuondoa umasikini hivyo italeta mshikamano na Maendeleo katika  Mkoa.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti