• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Maadhimisho ya Miaka 25 ya SAUT,kuja pamoja na kituo cha Ubunifu cha Sayansi na Teknolojia

Posted on: May 11th, 2023

**Maadhimisho ya Miaka 25 ya  SAUT kwenda pamoja na kuanzishwa kituo cha Ubunifu cha Sayansi na Teknolojia*


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima amesema Maadhimisho ya mwaka huu ya Miaka 25 ya Chuo Kikuu cha Mt.Augustino SAUT yatakwenda pamoja na kuanzishwa Kituo cha Ubunifu cha Sayansi na Teknolojia ambacho kitakuwa mkombozi kwa maendeleo ya vijana hapa nchini.

Akizungumza leo Ofisini kwake katika  Mkutano na Vyombo vya habari pamoja na uongozi wa chuo hicho Kikuu,Mkuu huyo wa Mkoa amesema ndani ya miezi miwili kituo hicho kitakuwa tayari kikijikita kwenye Kilimo,Uvuvi na Ufugaji na kitakuwa chuoni hapo.

Ameongeza kuwa tayari Serikali imeweka mazingira mazuri kwa vijana kwenye sekta ya Kilimo,Uvuvi na Ufugaji,hivyo kuwaongezea ujuzi zaidi kupitia kituo hicho kutaleta mapinduzi chanya katika maendeleo yao hasa kujiajiri wenyewe.

"Serikali ya Mkoa itatafuta maeneo kama pale shamba la mifugo la Mabuki tunaweza kuomba hekari kumi kwa ajili ya matumizi ya vijana kufundishwa Ufugaji bora na wa kisasa wa ng'ombe pia tutazishirikisha baadhi ya Halmashauri kutupatia maeneo rafiki ya Uvuvi na Kilimo,Amesisitiza Mhe. Malima.

Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha hatua hii itakiingiza Chuo cha SAUT kwenye sura ya kimataifa zaidi kwani mpango kama huu wa ubunifu umefanyika kwenye vyuo vingi maarufu Duniani kama Chuo Kikuu cha  Havard kilichopo Marekani.

"Mhe.Mkuu wa Mkoa nakuahidi yote uliyozungumza tunakwenda kuyatekeleza hasa hili la kuanzishwa hiki kituo,Wataalamu wa kufanya kazi hii wapo na kila kitu kitakwenda sawa na kukamilika kwa wakati,"Mhe.Balozi.Prof.Costa Mahalu,Makamu Mkuu wa SAUT.

Kilele cha Maadhimisho ya miaka 25 ya Chuo Kikuu cha Mt.Augustino  kitakuwa ni Novemba 11,2023 huku shughuli mbalimbali za ndani na nje ya Chuo hicho kuelekea Maadhimisho hayo zikianza Mei mwaka huu

SAUT kilianza kuwa Chuo Kikuu mwaka 1998 awali kilijulikana kama Nyegezi Social Training Centre.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti