• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

MAADHIMISHO YA WIKI YA MAZIWA KITAIFA YAENDANE NA HADHI YA MKOA WA MWANZA: RAS BALANDYA

Posted on: February 15th, 2024

MAADHIMISHO  YA  WIKI YA MAZIWA KITAIFA YAENDANE NA HADHI YA MKOA WA MWANZA: RAS BALANDYA


*Aitaka kamati ya maandalizi kuhakikisha yanafana na kuwa na tija kwa wana Mwanza*


*Aonesha imani ya mnyororo wa thamani kwa bidhaa ya maziwa kuzidi kuimarika Mwanza*


*Awataka wadau wa maziwa kulitumia jukwaa hilo kuwa wazalishaji bora wa bidhaa hiyo*

                                                                                                                                                    Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana leo Februari 15,2024 amefungua kikao cha kwanza cha maandalizi ya wiki ya kitaifa ya maziwa itakayofanyika mkoani humo kuanzia Mei 27 hadi Juni Mosi, 2024 na kuitaka kamati ya maandalizi kuhakikisha yanafana na kuwa na tija kwa wana Mwanza.

Akizungumza na kamati hiyo wakiongozwa na ujumbe kutoka  Bodi ya maziwa kwenye ukumbi mdogo wa Ofisi ya mkuu wa mkoa, Balandya amesema Wizara ya Mifugo na Uvuvi imefanya uamuzi mwafaka wa maadhimisho hayo kufanyika Mwanza kutokana na Mkoa huo kuzidi kuimarika kiuchumi na kuwa wa pili kuchangia pato la Taifa.

Amebainisha kutokana na hadhi ya Mkoa huo waandaaji wana wajibu wa kuhakikisha maadhimisho hayo yanayofanyika kila mwaka yanaacha fursa nyingi kuanzia kwa mfugaji, mlaji hadi kwa wafanyabiashara wadogo

"Pamoja na lengo la maadhimisho hayo kuboresha na kuhamasisha matumizi sahihi ya maziwa,yatakuwa msaada pia kwa wadau kupata fursa ya kuelimika namna ya kuboresha uzalishaji na kuweza kumudu soko la ushindani kwa ujumla.

Akitoa taarifa fupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi,mwakilishi wa Msajili wa Bodi ya maziwa Bw.Aggrey Nsemwa  amesema wiki hiyo ya maziwa itaambatana na shughuli mbalimbali kuelekea kilele chake Juni Mosi.

"Ndugu Katibu Tawala mkoa tutakuwa na kongamano kwa wadau wa maziwa lengo likiwa kubadilishana uzoefu na kusikia changamoto zao na kuzipatia ufumbuzi,pia tutakuwa na zoezi la ugawaji maziwa baadhi ya maeneo ikiwemo kwenye vituo vya kuwalea wazee,"amesisitiza Nsemwa.

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Emil Kasagara amebainisha mkoa wa Mwanza umejipanga vizuri kufanikisha wiki hiyo ya kitaifa ya maziwa kwa kushirikiana na bodi ya maziwa na kuwataka wananchi kutumia vizuri fursa hiyo.

Maadhimisho hayo ya 27 yanayofanyika kila mwaka mwishoni mwa Mei na kuhitimishwa Juni Mosi,mwaka jana yalifanyika Mkoani Tabora.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti