• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Maandalizi GLITE Yazinduliwa Mwanza

Posted on: March 4th, 2020

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamissi Kigwangala amezindua rasmi maandalizi ya maonesho ya kimataifa y a utalii katika Ukanda wa Maziwa Makuu na jukwaa la uwekezaji katika sekta hiyo,yanayotarajiwa kufanyika juni 19 hadi 21 mwaka huu,katika uwanja wa CCM Kirumba Mkoani Mwanza, ambapo aliwahamasisha wawekezaji wa ndani kutumia jukwaa hilo kama fursa ya kuvitambua na kuvitangaza vivutio vilivyopo nchini.

Akizungumza  wakati akizindua nembo maalum ya maonesho hayo ya kimataifa yaliyofanyika  jijini Mwanza yanayotambulika kwa jina la Great Lakes International Tourism Expo(GLITE) yanayolenga kuvitanganza vivutio vya utalii vya maeneo ya maziwa makuu yatakayokuwa yanafanyika kila mwaka ambayo yatahusisha mikoa ya Mwanza,Geita,Simiyu,Shinyanga,Kagera,Mara,Tabora na Kigoma Dkt.Kigwangala ,alisema ili kuhakikisha fursa ya utaliii inaenea kwa nchi nzima,kupitia maonesho hayo yatatangaza vivutio hivyo na kuwavutia wawekezaji ambapo wanatarajia kuweka mabanda zaidi ya 150 .

Alisema,zaidi ni kutangaza vivutio vilivyopo pamoja na kutangaza fursa mbalimbali ambazo zinapatikana katika mikoa hiyo hatimaye kuwataembeza wageni ambao watakuja kwenye maonesho ili washuhudie kwa macho kile kilichotangazwa na kuwaeleza taratibu za uwekezaji ambao watajitokeza ili waelewe kwenye ukanda huu kuna fursa zipi na taratibu zipoje za kupata maeneo ya kuwekeza.

“Mazao ya utalii ni vitu vingi kwa kiasi kikubwa Tanzania tunasifika kuwa na vivutio vya asilia mbapo hiyo ni bidhaa ya kwanza, ya pili hatujawai sana kutumia maji kama mazao ya utalii, kuanzisha sakta hii ya utalii kwa ukanda huu ya kutumia ziwa Victoria na Tanganyika maana yake tunatoa fursa ya watu kuona nini ni wanaweza wakafanya kupitia maziwa haya,linaweza kuwa zao la pili ambalo linaweza kutusaidia kuleta upekee katika ukanda huu,eneo la tatu ni  mila na desturi za watu wa maeneo haya,kabila yaliyopo hapa ni mengi  mfano Mkoa wa Mara una zaidi ya makabila 16 ambapo una kuta kijiji kimoja kabila hili kijiji kingine kabila jingine,pia kabila hili la wasukuma,tuna madini ya dhahabu na almasi,”alisema Dkt.Kigwagala.

Aidha alisema,ni jambo la msingi kwa hatua hiyo ya awali kwa ukanda huo kuzitambulisha fursa zilizopo ili zijulikane na kusaidia uelewa wa vivutio ili kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza na kuandaa miundombinu ya utalii ambapo ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi(CCM) ya mwaka 2015-2020 inazungumzia suala la kukuza utaliii na ielekeza wizara husika kuongeza watalii kutoka milioni 1 mwaka 2015 hadi milioni 2 mwaka huu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf  Mkenda, alisema maonesho hayo yanatarajiwa kuwa na washiriki kutoka nchi mbalimbali duniani zenye vivutio  zitapenda kuja  kutangaza vivutio vyao nchini hapa.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Nchini {TBB} Jaji Mstaafu Thomas Mihayo, alisema bodi hiyo ipo tayari kusimamia,kujitolea na kushughulika ili maonesho hayo ambayo ni ya  kwanza na ya aina yake yaweze kufanikiwa na kufanyika kwa ngazi ya kimataifa huku akiwahimiza wakuu wa mikoa hiyo inayohusika katika maonesho hayo kutangaza shughuli hiyo kila mara kuwa itafanyika mkoani Mwanza pamoja na watendaji wasekta hiyo wakijipange katika ufanyaji kazi.

Baadhi ya wakuu wa mikoa itakayoshiriki katika maonesho hayo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella na Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Gabriel wamesema wapo tayari kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kuibua na kuendeleza fursa za utalii zinazopatikana huku Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Emmanuel Maganga akitumia fursa hiyo kutoa ombi la kupatika naeneo  la kudumu kwa ajili ya kufanyia maonesho hayo.

“Sisi kama Mikoa tupo tayari tumejipanga kwa fursa zilizopo katika mikoa yetu,ili kuweza kushiriki katika matayarisho, lakini vilevile kuhamasisha wadau kutoka sekta mbalimbalia mbao ni wadau katika sekta ya utalii kushiriki kama ambavyo inatarajiwa mwisho wasiku  kutoa mchango wa kutosha kwa maendeleo ya mikoa yetu,watu wetu na nchi yetu kwa ujumla,”alisema Mhe.Mongella.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti