• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara aridhishwa na Miradi ya Kimkakati Mwanza

Posted on: September 5th, 2022


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Mhe. Abdurahman Kinana, ameridhishwa na namna ujenzi wa miradi ya kimkakati inavyoendelea Mkoa wa Mwanza kwa hatua iliyofikiwa na usimamizi wa miradi hiyo.

Mhe.Kinana ameyasema hayo mara baada ya kuwasili Mkoa wa Mwanza akitokea Mkoani Geita na kukuta ujenzi ukiendelea ndipo alipowasilisha salaam za Mhe.Rais akizungumza na wananchi, wataalamu na viongozi mbalimbali katika Mradi wa Daraja la J.P MAGUFULI lenye urefu wa km 3.2  linalojengwa na mkandarasi Kampani ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC ) kwa gharama ya zaidi ya Bilioni 700 na kutarajiwa kukamilika ifikapo Februari 2024, ndipo alipowataka watendaji kuendelea kusimamia miradi hiyo kwa weledi na ubora.

"Mhe.Rais amenituma niwasalimie,na anangoja aje kuwa Mgeni Rasmi  kufungua daraja hili,na siku ya kufungua daraja hili watachinjwa ng'ombe wengi sana, na siyo ng'ombe tu ng'ombe lazima aende na kinywaji,''alisema Mhe.Kinana.

Aidha, Mhe.Kinana aliongeza furaha yake alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali na wanachama wa chama cha Mapinduzi alipowasili Ofisi ya CCM Mkoa ambapo aliwashukuru wote kwa mapokezi mazuri na jinsi walivyomlaki na walivyojitokeza kwa wingi.

Vilevile Mhe.Kinana amekagua ujenzi wa Meli ya MV. Mwanza Hapa Kazi tu mradi unajengwa kwa Gharama ya Shilingi Bilioni 97 na kuridhika namna mradi huo unavyoendelea.

Pamoja na  kukagua uhai wa Chama cha Mapinduzi kwa kuzungumza na wanachama wa Chama hicho pamoja na wavuvi na vikundi vyao, Mhe.Kinana amekagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020/2025  kwa kutembelea mradi wa Soko Kuu Jijini hapo unajengwa na Kampuni ya Mohamed Builders Co.Ltd kwa gharama ya Shilingi Bilioni 20 huku ukitarajia kunufaisha wafanyabishara wakubwa na wadogo.

Hata hivyo, Mhe.Kinana aliwasili Mwanza  Septemba 4, 2022 na kupokelewa katika Kijiji cha Igaka, Kata ya Buzilasonga wilayani Sengerema mkoani Mwanza, huku akilakiwa na  viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa  wa Mwanza Mhe. Dkt. Athony Dialo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima, wanachama na wananchi wa Mkoa huo.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti