• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Maonesho ya 14 ya Biashara Afrika Mashariki Yafunguliwa Mwanza

Posted on: September 7th, 2019


Maonyesho hayo ya kimataifa yanayohusisha nchi za ukanda wa Afrika mashariki yamefunguliwa katika ukumbi wa Rock city mall Mgeni rasmi akiwa  Mkurugenzi mtendaji wa Tan-Trade Eng.  Edwin Luta kwa niaba ya waziri wa viwanda Mhe. Innocent Bashugwa, lengo likiwa ni kuboresha maonyesho hayo ili yaweze kupata sura rasmi ya kimataifa.

Akifungua maonyesho hayo Eng.Luta amezipongeza nchi za Afrika mashariki kwa kushirikiana pamoja  na kuandaa maonyesho yanayohusisha bidhaa tofauti tofauti kutoka katika nchi hizo ikiwemo vifaa vya ujenzi, nguo, pembejeo za kilimo, utalii na mawasiliano, vyombo vya jikoni, Elimu, madawa ya asili.

Kutokana na maonyesho hayo yatafanya wafanya biashara kupata fursa mbalimbali ili kuweza kukuza uchumi wetu na kuondoa tatizo la ajira katika nchi za Afrika mashariki.

"Madhumuni ya maonyesho haya ni kutoa fursa kwa wafanya biashara na makampuni yale ya ndani na nje ya afrika mashariki kutumia jiografia ya Mwanza katika kuongeza uwekezaji wa ukanda huu" Alisema Luta.

Aidha Eng. Luta amebainisha kuwa kutokana na maonyesho hayo kufanyika mara kwa mara yameweza kuwasaidia wafanya biashara wengi kujifunza ujuzi mbalimbali kutoka nchi jirani.

"Natoa wito kwa wafanya biashara na wawekezaji wazidi kuimarisha biashara na uwekezaji katika bidhaa tofauti, pia wito kwa viwanda vyote ili kuhudhuria katika maonyesho mengi ikiwemo maonyesho ya sabasaba ambayo ni ya kitaifa" Alisema Luta.

Mbali na huo wito Eng. Luta amesema kilimo chetu bado kinachechemea sana hivyo tunapaswa kusimamia matangazo ya biashara na ili tuweze kuzalisha zaidi tuwe na kilimo cha heka ili tuuze ndani na nje ya nchi yetu.

"Tanzania hatuwezi kutoka kwa kilimo cha jembe".

Naye Mwenyekiti wa  Tanzania chamber of commerce, Industry and Agriculture (TCCIA) mkoa wa Mwanza Dk. Elbariki Mmari amesema kutokana na mafanikio mbalimbali katika maonyesho hayo changamoto imekuwa kodi zisizo za halali kwa wafanyabiashara na stempu za wafanyabiashara kwani zinapatikana Dar es salaam tu.

"Naomba serikali iweze kuboresha huduma za stempu kwa kuweka makala katika mikoa mingine"Alisema Mmari.

Aidha Rais wa (TCCIA) taifa Mhe.Paulo Koyi amezungumza na kuwataka wafanya biashara na wawekezaji kuweka juhudi na jitihada zaidi katika biashara yao na kushiriki kwa pamoja katika kuleta maendeleo ya nchi yetu.

"Wafanyabiashara wafanye kazi kwa makini na juhudi ili kesho na kesho kutwa Tanzania iwe nchi mahiri katika biashara ikiwa na sura mpya katika maendeleo yetu na hata binafsi"Alisema Koyi.

Pamoja na hayo Eng.  Luta ametoa neno kwa wafanya biashara kwa kusema Tan-Trade imewaunga wanawake kuimarisha biashara iliyopo mipakani kwa kuunda taasisi mbalimbali ambapo asilimia 70 ya wanawake wanafanya biashara mipakani, na kutoa wito kwa serikali kuwawezesha kufanya biashara ambayo ni rasmi na kuwapongeza wanawake kwa hatua hiyo.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti