• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Matokeo Utafiti wa Afya ya Uzazi, Mtoto na Viashiria vya Malaria 2022 yaje na Mageuzi chanya kisekta: RAS Mwanza

Posted on: February 7th, 2024

Matokeo Utafiti wa Afya ya Uzazi, Mtoto na Viashiria vya Malaria 2022 yaje na Mageuzi chanya kisekta: RAS Mwanza


Leo Februari 7, 2024 Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana amefungua semina ya siku mbili ya utoaji wa matokeo ya Utafiti wa afya ya Uzazi na mtoto na Viashiria vya Malaria mwaka 2022 na kuwataka washiriki kuyatumia vizuri matokeo hayo ili yawe na tija kwenye sekta ya afya.

Akizungumza kwa niaba yake kwenye ukumbi wa mikutano Hotel ya Monarch, Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali watu, Daniel Machunda amesema Serikali ya awamu ya sita imefanya maboresho makubwa sekta ya afya hivyo changamoto za vifo vya mama na mtoto viepukike kwa kutumia matokeo ya utafiti huo.

Amewataka washiriki hao wengi wao wakiwa ni wataalamu wa afya kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa,kutambua kuwepo na vifo vinavyotokana na uzazi  vinachangia kupunguza nguvu kazi ya Taifa na mipango ya maendeleo  kwa ujumla.

"Naumia sana ninaposikia kumetokea kifo cha mama na mtoto, hili ni jambo jema (Uzazi) na lenye furaha ndani ya familia la mama kujifungua lakini lisije na taarifa mbaya, nawasihi sana ndugu washiriki baada ya semina hii mkalete mageuzi ya kweli kwenye maeneo yenu," amesisitiza Machunda kwenye ufunguzi.

Ameipongeza Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali kwa utafiti huo na hasa katika eneo la afya ambalo lina umuhimu wa pekee ndani ya Jamii na Taifa kwa ujumla.

"Kanda yetu ya Ziwa licha ya kufanya vizuri  wajawazito kuhudhuria kliniki kwa asilimia 91 lakini idadi ya wanaokwenda kujifungua kwenye vituo vya afya hairidhishi,pia utoaji wa chanjo tumefikia asilimia 51 tofauti na Ile inavyotakiwa na Serikali ya 53%, yote haya hatuna budi kwenda kuyafanyia kazi,"Katibu Tawala Msaidizi.

Mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali Emilian Karugendo amesema Taifa lolote Duniani haliwezi kuwa na maendeleo kama litakabiliwa na changamoto ya wananchi wake kuwa wagonjwa,kwa kutambua umuhimu huo Ofisi yake kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Wizara za afya Bara na Visiwani wamefanya utafiti huo na kutoa taarifa kwa Serikali kwa hatua zaidi.

Washiriki wa semina hiyo ni waganga wakuu wa mikoa,waganga wakuu wa wilaya,waratibu wa Malaria,na Maafisa mipango kutoka mikoa ya Mwanza,Shinyanga,Mara,Geita,Kagera na Simiyu.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti