• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Mhe. Mongella aweka jiwe la Msingi Kituo cha Afya Kamanga

Posted on: January 19th, 2018


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella ameweka jiwe la msingi Kituo cha Afya cha Kamanga  kilichojengwa kwa ushirikiano  baina ya Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na Shirika lisilo la Serikali  lijulikanalo kama  CEDAR FOUNDATION  lenye Makao Makuu yake Nchini Uswisi kwa Tanzania lina Ofisi  yake Jijini Mwanza.

Ujenzi wa Kituo hicho ulianza Februari 2015 na kumalizika Novemba 2017 ambapo ujenzi huu unafanyika kwa awamu, na kwa sasa limejengwa jingo la wagonjwa wan je lenye vyumba 23 na nyumba 9 za watumishi,hadi kukamilisha Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ilichangia Jumla ya Shilingi 59,126,098.50 ambapo kati ya hizo  52,693,000 zilitumika kutengeneza mfumo wa maji na Shilingi 3,800,000 ziliweka mfumo wa umeme  wakati  1,433,097.50 zilitumika kulipia hati miliki ya eneo na Shilingi 1,200,000 zilitumika kupima eneo la kituo.

Shirika la CEDAR FOUNDATION limechangia jumla ya Shilingi bilioni 2.325 ambapo   fidia kwa waliokuwa wakazi wa eneo hilo ni shilingi milioni 251, ujenzi ni shilingi bilioni 1.55, tofauti na ujenzi Shirika limetoa vifaa tiba vyenye thamani ya ya Shilingi milioni 331 ikiwa ni gharama ya vifaa hivyo na usafirishaji,pia imegharamia vifaa vya ofisi kama jenereta,mashine ya kuchomea taka hatarishi na kufunga mfumo wa kielektroniki kwa thamani ya shilingi milioni 193.

Mhe.Mongella awali akiwapongeza wafadhili hao amesema kuwa, Mradi huu unategemea kutoa huduma bora za afya na ustawi wa wananchi zaidi ya watu elfu 30 wa kata ya Nyamatongo na kata nyingine za jirani, hivyo utasaidia vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema.

 Mhe. Mongella ameongeza kuwa, pamoja na juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali pamoja na wadau wa maendeleo Ikiwemo CEDER FOUNDATION, Sekta ya Afya Mkoa wa Mwanza inakabiliwa na changamoto mbalimabli ikiwa ni pamoja na upungufu wa watumishi wa afya kwa asilimia 51,ukowefu wa vituo vya huduma katika vijiji 303 na uwepo wa majengo ambayo hayajakamilika 109 katika vijiji na baadhi ya ya vituo vya huduma, upungufu wa nyumba za watumishi wa afya 951,ukosefu wa mashine muhimu za uchunguzi katika Mkoa(MRI), mwitikio mdogo wa jamii kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF ambapo kwa sasa ni 10.89% ya waliojiunga  na o.71%(TIKA) lengo likiwa ni asilimia 30.

Hata hivyo, katika kukabiliana na changamoto hizi Mkoa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo unaendelea kuboresha miundombinu ya utoaji huduma za afya, ununuzi wa vifaa muhimu vya uchunguzi wa magonjwa, ufungaji wa mifumo ya kielektroniki katika vituo vyote vyenye umeme na kutenga nafasi za ajira kila mwaka.

Aidha, Mkoa umepokea Bilioni 2.62 kwa ajili ya upanuzi wa vituo vya afya Mkoani Mwanza hivyo utahusisha ujenzi wa majengo ya huduma za upasuaji wa dharura za uzazi, wodi za wazazi, maabara na nyumba za watumishi utakaotekelezwa katika vituo 6 vya afya, ambapo ujenzi wa awamu ya kwanza umeanza katika vituo viwili vya Kahangara –Magu  na Karume – Ilemela na awamu ya pili itahusisha vituo vya Afya vya Bwisya – Ukerewe na Malya – Kwimba, Kome- Buchosa na Kagunga – Sengerema.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti