• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Mikakati ya Maendeleo Yajadiliwa Buchosa

Posted on: September 22nd, 2019


Katika kutekeleza mikakati ya kimaendeleo inayofanywa na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,  Halmashauri ya wilaya ya Buchosa iliyopo  mkoani Mwanza ni mojawapo ya halmashauri iliyojipanga katika kutekeleza  mikakati hiyo.

Hayo yameelezwa  hii leo katika kikao cha 4 cha baraza la madiwani kilichofanyika Wilayani humo kilichoongozwa na mwenyekiti Idama Kabanzi diwani wa kata ya Nyanzeba na kuhudhuriwa na  madiwani, Wajumbe pamoja na mbunge  na viongozi mbalimbali wa halmashauri hiyo huku lengo likiwa ni kujadili ajenda mbalimbali za kutekeleza mikakati ya maendeleo katika halmashauri hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho,  kwa upande wa sekta ya afya mbunge wa halmashauri ya wilaya ya Buchosa Dkt. Charles Tizeba ameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuweza kujenga hospitali ya kisasa wilayani hapo ambayo inatarajia kuanza kutoa huduma ifikapo mwishoni mwa mwaka huu ambapo walengwa wakuu watakuwa akina mama wajawazito,  watoto pamoja na wananchi wote wa halmashauri ya wilaya ya Buchosa.

"Nipende kuishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutujengea hospitali hii ya kisasa ambayo inatarajia kuanza kutoa huduma ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. " Alisema Tizeba.

Naye, Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Buchosa, Bw. Chrispine  Luhanda ameeleza kuwa hospitali hiyo itakapokamilika wananchi wa Buchosa ambao wengi wanakwenda kupata huduma ya afya sengerema na geita ambapo wanatembea umbali mrefu watakuwa  wamesogezewa huduma hiyo kwa ukaribu zaidi.

"Matarajio yetu ni kwamba baada ya hospitali hii kukamilika wananchi wa halmashauri ya Buchosa watakuwa wamesogezewa huduma hii ya afya kwa ukaribu,  sababu wamekuwa wakienda kupata huduma hiyo sengerema, geita na wengine kuvuka hadi Mwanza. "Alisema Luhanda.

Aidha, diwani wa viti maalumu halmashauri ya wilaya Buchosa, tarafa ya ya Nyehunge Ndg. Mwamini Antony Gandama ameshauri viongozi  hao kuweza kutembelea miradi wanayoisimamia ili kuleta tija na matokeo ya pesa zinazotolewa na serikali yaonekane kwa wananchi wa halmashauri hiyo.  

" Nipende kuwashauri viongozi kuweza kutembelea  miradi wanayoisimamia ili ilete tija na matokeo ya pesa zinazotolewa na serikali  yaweze kuonekana kwa wananchi wa Buchosa. " Alisema Gandama.

Katika hatua nyingine Eng. Kassian Mwitike, Meneja wa usambazaji maji  sengerema amebainisha kuwa wameshaweka mikakati mbalimbali kwa kushirikiana serikali na kupitia vyanzo mbalimbali kukamilisha mradi wa maji wa Nyakalilo na Bukokwa ulioanza mwaka 2014  ambao umeshafikia asilimia 90% ya utekelezaji wake na kusema  utakamilika ifikapo mwezi disemba mwaka huu ili wananchi waweze kupata huduma ya maji.

"Kwa mikakati tuliyojipanga kupitia wakala wa usambazaji maji na usafi wa mazingira vijijini,  serikali na kupitia vyanzo mbalimbali tumejipanga kuhakikisha mradi wa maji wa Nyakalilo na Bukokwa ambao umeshafikia asilimia 90% ya utekelezaji wake kukamilika ifikapo mwezi disemba. " Alisema Mwitike.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa kikao hicho Idama  Kabanzi amewaomba wakurugenzi na viongozi wote kuhakikisha wanakaa kwenye nafasi nzuri ya kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili halmashauri ya Buchosa ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na changamoto hizo.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti