• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

MIRADI YA ZAIDI YA BILIONI 100 KUFIKIWA NA MWENGE WA UHURU MWANZA

Posted on: August 24th, 2025

Leo Agosti 24, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameupokea Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa shule ya msingi Muluseni wilayani Ukerewe ukitokea Mkoani Mara na amebainisha kuwa utakimbizwa kwa siku 8 katika miradi 57 yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 100.

Amefafanua kuwa katika miradi hiyo 57, 11 itawekewa mawe ya Msingi ikiwa na thamani ya Tshs. 36,879,656,520.00 miradi 30 thamani ya Tshs. 12,978,562,557.50 itazinduliwa ambapo 10 yenye thamani ya shs. 2,475,460,130.90 itafunguliwa na miradi 9 yenye thamani ya Tsh.48,632,209,710.00 itakaguliwa.

Amebainisha kuwa Mwenge wa Uhuru mkoani humo utakimbizwa umbali wa kilometa 722 katika eneo la nchi kavu na majini (nautical mile) 45 katika miradi iliyo kwenye sekta za maji, barabara/madaraja, elimu na afya.

Maeneo mengine ametaja kuwa ni kwenye  huduma za kiutawala, kijamii na kiuchumi kwa maendeleo ya wananchi na utawala bora, uhifadhi wa mazingira na utumiaji wa nishati safi na salama, usafi na utunzaji wa masoko na kuzuia na kudhibiti na kuzuia vitendo vya ukatili.

Kadhalika, ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa 2025 kwa amani na utulivu kama ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru usemavyo “JITOKEZE KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025 KWA AMANI NA UTULIVU”.

Katika wakati mwingine, Mkuu wa Mkoa amemkabidhi mwenge wa uhuru Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Mhe. Christopher Ngubiagai kwa ajili ya kuukimbiza katika miradi 8 ya maendeleo leo Agosti 24, 2025.

Mkoa wa Mwanza baada ya kukimbiza mwenge wa uhuru kwa siku nane kuanzia tarehe 1 septemba, 2025 utakabidhiwa Mkoani Geita katika viwanja vya shule ya sekondari ya Lwezera wilayani Geita.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti