• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Mkoa wa Mwanza wampongeza Mhe Rais Samia kwa kuboresha maslahi ya Wafanyakazi

Posted on: June 1st, 2022

Mhe. Mhandisi Robert Gabriel, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ametoa rai kwa wafanyakazi wa taasisi na idara za serikali mkoani humo kufanya kazi kwa bidii, uzalendo na weledi ili kuuletea maendeleo Mkoa huo na Taifa kwa ujumla.

Ameyasema hayo leo kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa baada ya kupokea maandamano ya azimio la kumpongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha maslahi ya watumishi kutoka kwa shirikisho la vyama vya wafanyakazi mkoani humo.

"Twendeni tukafanye kazi kwa uzalendo, itatuletea heshma kwa Mungu na kila mmoja akitekeleza majukumu yake tutakua tumemrudishia shukrani Mhe. Rais kwa vitendo na tusionekane kwenye wizi, ubadhirifu wala rushwa na haki ikainue maisha yetu."

Aidha, Mhe. Mkuu wa Mkoa amewashukuru wafanyakazi hao kwa utashi wao kuthamini mema aliyoyafanya Mhe. Rais kwao kupitia utumishi wao na kwa pamoja wakaamua kutoa kauli ya kumpongeza kwa maandamano yenye furaha na bashasha.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe.Amina Makilagi amesema Serikali ya awamu ya Sita  itaendelea kuwa sikivu hivyo ni wajibu wa kila mfanyakazi kufanya kazi kwa bidii katika eneo lake.


Akisoma risala ya Wafanyakazi Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Mkoani Mwanza TUCTA,Zebedayo Athuman amesema shukurani ya Wafanyakazi kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ni kuchapakazi kwa bidii kwa lengo la kuliletea Maendeleo Taifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi  Mkoani Mwanza,TUCTA  Yusuph Simbaulanga ameishukuru Serikali inayoongozwa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusikia kilio cha Wafanyakazi kitendo kitakachoongeza ari ya kazi.


Vilevile, Mhandisi Gabriel amewasihi viongozi wa wafanyakazi kushughulikia mara moja changamoto za wafanyakazi na kuwasilisha kwake zile zinazohitaji msaada zaidi wa ofisi yake na akaahidi kutoa ushirikiano.

"Kwa  mema yote haya yaliyofanyika tunalo deni kwa Mhe. Rais hivyo niwaombe viongozi wa shirikisho na viongozi wa vyama vya wafanyakazi isiwepo kero ya mfanyakazi yeyote bila kuifanyia kazi na kama kuna changamoto yoyote nitaifanyia kazi ili mfanyakazi yeyote akifika asubuhi kazini aanze kwa sala ya shukrani kwa mwenyezi mungu." Amesema Mkuu wa Mkoa.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti