• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Mkono wa pole wahanga MV nyerere waendelea kutolewa,zoezi la kuondoa meli majini,uopoaji miili

Posted on: September 25th, 2018


Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mwasiliano Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe amesema zoezi la uopoaji wa miili ambayo itakua imenasa na kugeuza kivuko na kukitoa majini bado linaendelea likiongozwa na jeshi la wananchi kwa kishirikiana na majeshi mengine.

“Mpaka kufikia jana meli ilikua imelala kifudifudi na sasa kimelala ubavu na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo akiongoza zoezi hili,” alisema Kamwelwe.

Pia amewashukuru watanzania mbali mbali  walioguswa na wanaoendelea kuombea shighuli zinazoendelea Ukara.

Aidha zoezi la kupokea michango bado linaendelea ambapo wadau mbalimbali wanaendelea kujitokeza katika kichangia wananchi wa Ukara waliopatwa na Janga hili, miongoni mwa wadau walio wasilisha michango yao ni Baraza la maaskofu Jimbo la Dar es Salaam wameweka kwenye akaunti ya maafa kiasi cha shilingi Milioni 25. Na Benki ya KCB Tanzania Zuhura Muro nayo imetoa kiasi cha Shilingi Milioni 125 pesa imeshawekwa kwenye akaunti tayari. Nao Benki ya Shirika la Posta limeweka Milioni 10.

Kwa siku ya leo imepokelewa Milioni 160, Hivyo mpaka saa sita mchana fedha zilizochangwa zinafanya jumla ya shilingi  557,020,000/-

Mkuu wa Majeshi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo amesema zoezi la kugeuza bado linaendelea vizuri na matumaini ya kugeuza kivuko ni mazuri mafundi na wataalamu wanaendelea kufunga Air Bags (maputo magumu yenye hewa) ili kisaidia kivuko kisimama. Na wakati zoezi hilo lilipokua linaendelea maiti moja ikapatikana. “Tunaendelea na kazi mpaka itakapo kamilika” Mabeyo.

Mtanzania mmoja anaitwa Abel Michael amewasilisha kiasi cha 100,000/- na mwenzake John Salia ametoa 200,000/-.

Katika hatua nyingine zoezi la kutambua miili linaendelea ambapo kuna familia moja iliyoweza kufika na kutambua ndugu yao aliyefariki miongoni mwa ile miili minne iliyokosa ndugu yao. Baada ya mahojiano ya masaa matano na ofisi za utambuzi wakaridhiwa kuwa yule aliyezikwa ni ndugu yao hivyo familia imeonyeshwa kaburi namba 8. Alisema Adam Malima Mkuu wa Mkoa wa Mara anaesimamia utambuzi wa miili katika kituo cha afya Bwisya katika kipindi hiki cha ajali.

Zoezi la Kulipa wafiwa na manusura wa ajali limeanza na fedha zinazotumika ni hii iliyochangwa na watanzani.

Michango inaendelea kutolewa wadau mbali mbali wanaendelea kutoa kama Kanisa la EAGT  waliotoa shilingi Milioni 5. Uwanja wa Ndege KIA Milioni 5, ATCL Milioni 10, River oil milioni 2, Olympic Oil milioni 10.

Jumla mpaka sasa ya fedha zote ni 589,320,000/=.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti