• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Mongella aonya watumishi wasio waadilifu

Posted on: February 15th, 2020

Watumishi wasio waadilifu wazidi kuididimiza Wilaya ya Ukerewe baada ya kubainika kuhusika  na wizi wa fedha za mapato wakati wa ukusanyaji kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vinavyoingiza mapato.

Akizungumza katika kikao cha majumuisho kilicho hudhuliwa na baadhi ya Madiwani, Wakuu wa idara, Kamati ya Ulinzi na Usalama na watumishi wa Halmashauri baada ya ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella katika visiwa 38 vya Wilaya hiyo alisema hali ya Wilaya hiyo haina unafuu wowote, kila alipopita wanasema wanalipa kodi lakini wakiulizwa fedha zilipo hazijulikani.

Alisema kuna wizi unaoendelea watu wanatumia visiwa kama fursa ya kuiba mapato hivyo hawataweza kuwaacha, wataanza na kufunga mianya yote ya ulaji, watendaji warudi kwenye mstari na wasikubali kudanganywa na vitu vidogo bali wasimamie haki na utaratibu na kuacha kuhujumu mapato kwa kuwa imebainishwa uwepo wa mapato mengi hadi sasa hayajaingizwa kwenye mfumo.

“Yeyote atakaye thibitika kuwa ni tatizo atang’oka mnaweza mkaishi kwa kuiba?..tunapita kwa wananchi tumekuta wamejenga madarasa, lakini Halmashauri haifanyi chochote hata kuezeka wameshindwa kodi mnakusanya lakini hata kuwarudia wananchi mkajenga vyoo hamna, kazi yenu ni kuchukua hela kila tunapopita wananchi wanaimba halmashauri..halmashauri yenyewe haionekani.”alisema Mongella.


Hivyo aliahidi kuanzisha mfumo wa kufanya  ukaguzi kila wiki kwa kipindi cha miezi sita huku akipiga marufuku kutoa fedha zitokanazo na mapato nje ya mfumo wa serikali kwa sababu utumiaji wa mapato nje ya mfumo ni tatizo sugu kwa Wilaya hiyo na ndiko mapato yanapopotelea .


Mongella aliagiza wapange safu mpya ya ukusanyaji mapato itakayoshirikiana na timu itakayotoka Mkoani kuja kuunga nguvu na kuifanya mifumo yote irudi kwenye mstari pia aliwataka watumishi kujituma na kufanya kazi kwa moyo ili kuchochea maendeleo.


Naye Mkuu wa Wilaya hiyo Cornel Magembe alisema Rais aliweka dhamana ili kuhakikisha anaisimamia Wilaya hiyo, hivyo alimtaka Mkurugenzi kubadilika na kuwa mkali ili watumishi wamtambue yeye ni nani, inaumiza sana wakati mwingine mkurugenzi  anaitisha kikao cha CMT watakaotokea ni watu wanne wengine watakuwa wanapita pembeni wala wasisikilize kinacho jadiliwa, asipobadilika miradi iliyopo itamshinda.


Kwa upande wake Mbunge wa jimbo hilo Joseph Mkundi alisema watumishi wasipoweza kujitambua na kujua wajibu wao ni upi kutaitajika nyenzo za ziada kufanya wawajibike kwenye nafasi zao ili kutimiza wajibu na kuitendea haki taasisi.


“Tuna fursa nyingi sijui tuna kwama wapi, lazima tujitoe mhanga na kuwa makini katika majukumu yetu” alisema Mkundi.


Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo George Nyamaha ameahidi kushirikiana na wataalamu ili kumaliza tatizo  hilo na kuwataka watumishi kubadilika katika suala la ukusanyaji wa mapato na wasitangulize sana posho kuliko kujitolea kutenda kazi yenye kuleta tija na maendeleo.


“Hatukuwa na nia mbaya kwenye ili jambo lakini sijui hii changamoto itaweza tusaidia tukatoka kama inawezekana siku moja hawa watu wa makao makuu wakiondolewa hii sheria ya kuwa mtu akitoka lazima alipwe posho labda hapo tunaweza tukabanana vizuri mimi ninafanya kazi nyingi ya kujitolea hawa wenzangu wanamishahara lakini unaweza kumwambia mtu toka nenda na asiende kwa sababu hajalipwa posho ya kutoka”alisema Nyamaha.



Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti