• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC Mongella apokea vifaa vya kujikinga na Corona Mwanza

Posted on: April 16th, 2020


Wadau wa Maendeleo na Taasisi mbalimbali za maendeleo zimetoa vifaa mbalimbali vikiwemo meza, ndoo, sabuni, diaba na matenki ya maji kwa ajili ya kusaidia kwenye mapambano ya Corona.

Vifaa hivyo vimepokelewa  jijini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella ambaye amezishukuru taasisi hizo na wadau hao wa maendeleo kwa moyo wa kujitoa katika kuunga mkono juhudi za Serikali kwenye mapambano ya ugonjwa wa homa ya mapafu( Corona) ambalo kwa sasa ni janga la dunia.

Aidha Mhe.Mongella amewataka wadau hao wa maendeleo kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto kwa kuweka mazingira yao katika hali ya usafi, kwa kunawa mikono kwa maji na sabuni kwa kutmia vitakasa mikono.

“ Nawashukuru sana wadau kwa kutoa vifaa hivi na kwa baadhi ya maeneo mmeshiriki pia kutoa chakula, lakini pia niwashukuru sana viongozi wa dini mnafanya kazi kubwa sana, kwa mahubiri na mafundisho yenu juu ya hili janga la Covid -19,” alisema na kuwataka wadau wengine zaidi kujitokeza kwa ajili ya kutoa vifaa vingine zaidi.

Mhe.Mongella ameongeza kuwa  ugonjwa wa Corona ambao unaenea kwa kasi hivi sasa duniani ni hatari sana kwa maisha ya binadamu na kuwataka wananchi na watalaam kutofanya uzembe wa aina yoyote kwenye mapambano ya Corona.

“ Niwaombe viongozi wa dini, mashirika na taasisi zote tuendelee kuelimisha na kuwahamasisha wananchi namna ya kuendelea kuchukua tahadhari,” alisema na kuwashukuru Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi watendaji, maafisa tarafa, madiwani na viongozi wa mitaa, vitongoji na vijiji kwa jinsi wanavyoendelea kujitoa katika kuwahamasisha wananchi namna bora ya kupambana na ugonjwa huo.

Akizungumza kwa niaba ya wadau waliokabidhi vifaa hivyo Mwakilishi kutoka Taasisi ya Hindu Nilesh Popat alisema wao wameamua kutoa vifaa hivyo ili kuunga juhudi za Serikali kwenye mapambano ya Corona.

“Mhe. Mkuu wa mkoa tumekuwa tukitembea mitaani bado tunaona mahitaji ni makubwa ya vifaa vinavyohitajika na ndiyo maana tumeamua kutoa vifaa hivi,” alisema Popat.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RMO) Dkt. Thomas Rutachuzibwa alizishukuru taasisi na wadau hao wa maendeleo kwa misaada ya vifaa hivyo ambayo itawawezesha wananchi kujikinga zaidi na maambukizi ya Corona.

Kwa upande wake Shehe Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Hassan Kabeke aliwataka watanzania kuendelea kumuomba Mungu ili awanusuru na  janga hili la ugonjwa wa corona.

“ Tunawaombea pia hawa waliotoa misaada yao na tunataka watanzania waendelee kuchapa kazi huku wakijikinga na ugonjwa wa corona,” alisema.

Baadhi ya taasisi na mashirika yaliyotoa misaada hiyo ni taasisi ya Hindu Union Temple iliyotoa chupa 28 za 500 mls za sabuni za kunawia mikono, Nyanza Roads Network iliyotoa ndoo 100 za plastic za lita 20 zenye koki, Siri Guru Sigh Sabha ambao wametoa meza 10 za chuma, tenki 10 za lita 250 kila moja na viti 5-0 vya plastic.

Taasisi nyingine zilizokabidhi vifaa ni pamoja na Cocacola Company iliyotoa madumu 100 ya lita 20 kila moja na Henan Afro –Asia Geo Engineering Company iliyotoa barakoa 200, deto sabuni zenye ujazo wa  lita moja nne, vitakasa mikono chupa 48 kila chupa ikiwa na mls 250.


Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti