• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Mwanza Bingwa tena Umitashumta Kitaifa

Posted on: June 29th, 2018

  

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Malima amehitimisha mashindano ya 23 ya Michezo ya UMITASHUMTA Kitaifa yaliyofanyika Mkoa wa Mwanza akimuwakilisha Waziri wa Nchi 0fisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo ambapo Mkoa wa Mwanza kwa mara ya pili mfululizo umeshika nafasi ya kwanza kitaifa.

Awali akihutubia katika kufungwa kwa mashindano hayo  Mhe.Adam Malima aliwashukuru wote waliofanikisha zoezi hilo hadi kufikia kilele juni 29 na kuwaasa  waendelee kufanikisha michezo katika shule zote Nchini.

 "Napenda kuchukua nafasi hii ya pekee kabisa kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa wa Mwanza kwa uongozi wake imara uliofanikisha mashindano haya kufanyika kwa amani na usalama katika muda wote ambao mashindano haya yamefanyika," alisema Malima.

Vile vile hakusita kumpongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dokta John Pombe Magufuli kwa juhudi kubwa zakikisha  kufanikisha kuwepo kwa mashindano hayo ambayo ni fursa pekee kwa vijana hao, katika kuonyesha vipaji vyao.


Mhe. Malima aliwasisitiza wanamichezo na wadau mbalimbali wa michezo kuhakikisha wanaienzi kauli mbiu ya mwaka huu  inayosema, "Michezo Sanaa na Taaluma ni Msingi wa Maendeleo ya Mwanafunzi katika Taifa letu.”


Katika mashindano hayo Mkoa wa Mwanza umeibuka kidedea na kuwa mshindi wa kwanza kwa ujumla huku Mkoa wa Ruvuma ukishika nafasi ya mwisho Kitaifa kwa mwaka huu,ambapo  Mwanza imekuwa bingwa kwa ya pili mfululizo huku katika mchezo wa netiboli wakifanya vizuri zaidi.

Naye Mwalimu Rehema Maruzuku ambaye ndiye kocha wa netiboli aliuzungumzia Mkoa wa Mwanza kwa nafasi ya pekee.

"Kwa netiboli Mkoa wa Mwanza umeshika nafasi ya kwanza kwa miaka mitatu mfululizo na ninafikiri kombe hili ni la Mkoa huu moja kwa moja kwa sababu ukimiliki kombe hili kwa miaka mitatu mfululizo basi ni la kwako"alisema Maruzuku.

Kwa upande wake  mwalimu Tibu kutoka Singida hakusita kutoa maoni yake juu ya uendeshwaji mzima wa mashindano hayo.


"Mashindano ya UMITASHUMTA yameendeshwa vizuri, sema kuna baadhi tu ya Mikoa bado hawajazingatia sana suala la umri kama tumeamua kuwachezesha tu watoto wa umri fulani basi tuwalete watoto sahihi katika umri uliopangwa,"alisisitiza Mwalimu Tibu.


 Nao wanafunzi waliouwakikisha vyema Mkoa wa Mwanza hawakusita kueleza siri ya mafanikio yao iliyowawezesha kutwaa ubingwa huo ambayo ni nidhamu nzuri,kufuata maelekezo ya walimu wao na waliongeza kuwa wamejifunza vitu vingi sana huku michezo ikiwaongezea ujasiri wa kujiamini kama wana michezo, na kufanya wapate marafiki wapya na kusisitiza kuwa mwakani watafanya vizuri zaidi, ambapo mashindano hayo yatafanyika Jijini Dodoma mwakani 2019.


Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti