• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Mwanza yaja na Muarobaini wa Madini Chumvi

Posted on: May 11th, 2023

**Wiki ya madini Mwanza yaja na mwarobaini wa madini chumvi*

*


Maonesho ya wiki ya madini yaliyofanyika kitaifa mkoani Mwanza kuanzia Mei 3 hadi 9, 2023 yamekuwa na faraja kwa wachimbaji  na wafanyabiashara ya madini ya chumvi nchini baada ya kupitishwa kwa maazimio 14 ya kuendelea sekta ya madini ikiwemo madini hayo.

Akizungumza jijini hapa jana baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania(Femata) John Bina alisema maazimio hayo yamepitisha na wadau mbalimbali walioshiriki mkutano huo, wiki ya madini na kongamano la madini lililofanyika Mei9,2023.

“Tumepitisha maazimio 14 kati ya hayo maazimio 10 yameilenga serikali kupitia Wizara ya Madini na manne yanailenga Femata yote yatafanyiwa kazi ili kuwanufaisha wachimbaji,miongoni mwa maazimio ni wizara ya Madini

kuandaa mkutano mkuu wa  kitaifa utakaojadili changamoto na fursa zilizopo kwenye uchimbaji na biashara ya madini ya chumvi nchini.

“Madini haya yamesahaulika sana, licha ya umuhimu wake kwenye mwili wa binadamu lakini yamekuwa hayapewi kipaumbele wakati tunayo mengi hapa nchini hivyo tunaamini hatukukaa hapa Mwanza kwa kwa siku nane bure siku hizo zitazaa matunda,” alesem Bina na kuongeza

 “Wachimbaji wa madini hayo na wafanya biashara watakwenda kunufaika kwa sababu serikali ikitambua changamoto na fursa zilizopo kutoka kwa sisi wachimbaji itazifanyia kazi maana serikali yetu inatusikiliza siku zote sisi wachimbaji wadogo na lengo letu la la kuchangia pato la taifa kwa asilimia 20 ifikapo mwaka 2028 tutalifikia,”alisema Bina

Maazimio mengine yaliyopitishwa ni pamoja na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kuendelea kufanya utafiti wa madini kwenye maeneo ya wachimbaji wadogo wa madini na taarifa za tafiti ziwafikie wadau kwa wakati, mchakato wa utoaji  leseni kwa wachimbaji wadogo uwe wa wazi na unaozingatia sheria, kanuni na taratibu ili kuendana na haki kwa wachimbaji wadogo wanaoomba leseni kupitia Tume ya Madini.

Pia Wizara ya Madini  kukamilisha zoezi la kupitia tozo zinazotozwa na halmashauri kwa wachimbaji wadogo ili isiwe kikwazo  katika uchimbaji mdogo wa madini .

Aidha Bina aliishukuru Serikali ya Mkoa wa Mwanza inayoongozwa na Mhe. Adam Malima  kwa  usalama waliopata muda wote wa siku tisa walipokuwa mkoani humo   .

Mgeni rasmi aliyefunga mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama cha  Wachimbaji Madini Wanawake Tanzania, (TAWOMA) Taifa Semeni Malale, alisema ili Femata iweze kutimiza malengo iliyojiwekea  ni vyema  wanachama wote wakashirikiana na kusameheana huku wakifanya shughuli zao kwa kumtanguliza Mwenyezi Mungu.



Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti