• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Mwenge wa Uhuru wataka taratibu za Miradi zifuatwe Wilayani Misungwi

Posted on: July 13th, 2022

Katika kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi na viwango elekezi viongozi wenye dhamana ya usimamizi wa miradi wametakiwa kufuata maelekezo ya miradi mbalimbali yanayotolewa  kuhusu miradi hiyo ili kuepuka maswali mengi yanayoleta wasiwasi wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo.

Hayo yamesemwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndugu  Sahili Geraruma mapema hii leo mara baada ya kukagua miradi inayopitiwa na Mbio za Mwenge Wilaya ya Misungwi.

Akiwa katika Shule ya Sekondari Manawa ambapo amekuta Ujenzi ukiendelea katika mradi huo uliogharimu shilingi milioni 471.8, ndugu Geraruma amewataka wenye dhamana ya usimamizi wa miradi kufuata taratibu zilizowekwa.

"Viongozi na wasimamizi wote wa miradi, hakikisheni  mnafuata taratibu zote zinazotakiwa kuhusiana na miradi ikiwemo kuomba kuongezewa muda pale,mnaposhindwa kukamilisha kwa wakati na siyo kukaa kimya,''amesema Geraruma.

Aidha,ameshauri na kuwataka Viongozi wa Halmaahauri hiyo kusimamia vizuri Miradi ambapo amepongeza baadhi ya Miradi hiyo ikiwa ni pamoja na Miradi ya sekta ya Afya, Elimu, Maji, Uwezeshaji Wananchi kiuchumi na Mradi wa Ujenzi wa Barabara.

Pamoja na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa kuhusiana na Miradi hiyo, Miradi iliyowekewa jiwe la Msingi, na kuzinduliwa ni pamoja na Ujenzi wa Shule ya Sekondari Manawa, Ujenzi wa Barabara ya Lami, Ujenzi wa Kituo cha Afya Usagara, Mradi wa Ujenzi wa Chuo cha Afya MacWish, Mradi wa usambazaji Maji wa Fella, Ujenzi wa Madarasa 8 katika Shule ya Sekondari Sanjo, na Mradi wa  usafi wa mazingira na usafirishaji mizigo.

Hata hivyo,Miradi hiyo imetokana na mchango wa jamii  shilingi Milioni 11.3 na Halmashauri imetoa shilingi Milioni 16.7 ambapo Serikali Kuu imechangia shilingi Bilioni 1.6 na wahisani wamechangia shilingi Bilioni 1.5 na Miradi yote inaendelea kutekelezwa na baadhi imekamilika.

Akihitimisha ukaguzi wa miradi  Geraruma amewataka wenye dhamana ya miradi hiyo kuhakikisha wanafanya marekebisho katika mapungufu yote yaliyobainika wakati wa ukaguzi ikiwa ni pamoja na kufuata na kuzingatia kanuni taratibu za Ujenzi ili kukamilisha Ujenzi huo na kupata Miradi inayokidhi na yenye Viwango.

Mwenge wa Uhuru utaendelea na mbio zake katika Halmashauri ya Wilaya ya Magu kesho tarehe 14/7/2022 baada ya kukamilisha mbio hizo Wilaya ya Misungwi  ukitokea Wilayani Kwimba ambapo umekimbizwa km 75.3 na kupitia miradi 7 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.12.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti