• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Nyamagana Yaahidi Milioni 200 kwa Vikundi

Posted on: August 9th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Dtk. Philis Mishack Nyimbi ameahidi kutoa millioni 200 kwa wafanya biashara wadogo wadogo  ili waweze kujiongezea mitaji  na kuendelea kuchangia uchumi wa nchi.

Mhe.Dkt.Nyimbi ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi katika soko kuu la Mwanza pamoja na wafanyabiashara wadogo wadogo aliowakuta katika eneo hilo.

"Naahidi kutoa cheki ya millioni 200 kwa wafanya biashara wadogo wadogo na wajasiliamali ambapo fedha hiyo inatoka Halmashauri ya jiji la Mwanza  na itagawiwa kwa vikundi mbalimbali vya kina mama, vijana na walemavu hivyo itasaidia kuleta  maendeleo katika jamii," alisema Mhe. Dkt.Nyimbi.

Hata hivyo Mhe.Dkt Nyimbi aliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa na Wilaya kama Sehemu ya kujitambulisha kwa wananchi na kutembelea  miradi mbalimbali ya maendeleo.

Naye Mhe. Mongella katika ziara hiyo amesisitiza swala la usafi,usalama pamoja na kufanya kazi kwa juhudi kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kuondoa maisha magumu kwa wananchi na kuongeza kipato cha familia na nchi kwa ujumla.

"Nahitaji ushirikiano kutoka kwenu zaidi, pia nawapongeza wamachinga kwa kuleta amani na utulivu kwenye jiji letu la Mwanza kwa kupunguza uhalifu kwani mnatupa ushirikiano mkubwa, hata hivyo nahitaji zoezi la usafi la kila Jumamosi liendelee ili kuepuka ugonjwa wa kipindupindu.

Aidha ameongeza kuwa kwa kuendeleza kauli ya Mhe. Rais Dkt. John Magufuli kila mtu ajitume kwa nafasi yake na kufanya kazi kwa bidii kwani Mhe.Rais anasema "Hapa kazi tu."

Mhe. Mongella aliwasisitizia swala la kulipa kodi kwa kila mfanya biashara hata kama ni kiasi kidogo kwani kwa kufanya hivyo wanachangia maendeleo ya nchi.

 Mhe. Mongella  alitembelea pia shule ya Nyakato B  na kuongea na wanafunzi ambapo amewasisitiza kusoma kwa bidii ili kuweza kufikia malengo yao na alitoa zawadi ya fedha kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na la tatu waliojibu  maswali yake kwa ufasaha ili kununulia madaftari na kalamu.

Hata hivyo kamati ilimalizia ziara hiyo kwa  kutembelea  Zahanati ya Isebanda, Wasambazaji wa dawa  za kilimo na mifugo( Twiga Chemical Industries),  pamoja na Shule ya Nyakato B.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti