RAS BALANDYA AKUTANA NA AFISA UCHAGUZI MWANDAMIZI KUTOKA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Leo Septemba 17, 2025 Afisa Uchaguzi Mwandamizi kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Yohana Mcharo akiwa na timu yake wamemtembelea Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ofisini kwake wakiwa na adhma ya kujitambulisha na kutambulisha uwepo wa Tume na majukumu ambayo watakuwa nayo katika Mkoa wa Mwanza hasa masuala ya uchaguzi.


