• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RAS BALANDYA ATAKA MIRADI YA MAENDELEO KUKAMILIKA KWA WAKATI

Posted on: June 17th, 2025

RAS BALANDYA ATAKA MIRADI YA MAENDELEO KUKAMILIKA KWA WAKATI


Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndugu Balandya Elikana ameziagiza Halmashauri za Mkoa huo kuweka utaratibu wa kutenga fedha na kupeleka kwenye miradi ya maendeleo ili ikamilike na huduma ziweze kutolewa kwa jamii.

Katibu tawala ametoa maagizo hayo leo tarehe 17 juni, 2025 wilayani Kwimba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wakati akiongoza baraza maalum la hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa halmashauri hiyo katika mwaka wa fedha unaoishia juni 30, 2024

Balandya amesema ukamilishaji wa miradi unasaidia pia kuokoa fedha ambazo zimewekezwa kwenye uanzishwaji hivyo si vema kutokamilisha ujenzi mathalani wa shule Nyamilama (401 M) ambao halmashauri imepeleka 205 pekee kwani ni sawa na kutupa fedha.

Vilevile, ametumia baraza hilo kuwakumbusha kuwa ni matakwa ya kisheria yanayotaka kupelekwa kwa fedha asilimia 40 ya mapato yote yanayokusanywa kutoka kasma ya mapato ya ndani.

Naye, Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija ameliasa baraza hilo kujenga tabia ya kufanyia kazi hoja za CAG zinapoibuliwa kwa kuwasilisha nyaraka zinazohitajika kisheria kama vile viambatisho na ushahidi wa manunuzi ili kujenga halmashauri hiyo kwa pamoja.

"Watendaji wenzangu kila mmoja wetu akatimize wajibu wake, tukashirikiane kwenye kazi zetu kila siku ili kuijenga halmashauri yetu kwahiyo daima tuwe wamoja na nawatakia kila la kheri kwenye uchaguzi", amesema Balandya.

Akitoa taarifa ya ukaguzi, Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Nje Mkoa wa Mwanza ndugu Henry Chausa amebainisha kuwa halmashauri hiyo ilifanyiwa ukaguzi kwa mwaka unaoishia juni 2024 na kupata hati inayoridhisha na kwamba kwa miaka mitatu mfululizo imepata hati hiyo.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti