• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RAS BALANDYA ATANGAZA MATOKEO YA DARASASA LA SABA KANDA YA ZIWA, MWANZA YANG'ARA

Posted on: June 13th, 2024

RAS BALANDYA ATANGAZA MATOKEO YA DARASASA LA SABA KANDA YA ZIWA, MWANZA YANG'ARA


Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana leo Juni 13, 2024  ametangaza matokeo ya Mtihani wa Utamilifu kwa darasa la Saba Kanda ya ziwa huku Mwanza ikiing'ara kwa ufaulu wa asilimia 84.6 kwa jumla ya wanafunzi 219,655 waliofanya mtihani huo.

Akitangaza matokeo hayo kwa niaba ya Makatibu Tawala wa Mikoa 5 ya Kanda ya ziwa, Elikana amebainisha kuwa nafasi ya pili imekwenda Mkoa wa Simiyu waliopata ufaulu wa 81%  ikifuatiwa na Geita wenye ufaulu wa 72.6%,wakati Kagera wakiwa nafasi ya nne ya ufaulu wa 62.4% na Mara wakiwa na 52.8%.

"Rai yangu kwenu Maafisa Elimu mliohudhuria hafla hii tuzidi kuongeza bidii kwani takwimu zinaonesha masomo matatu ya Hisabati, Kiingereza na Sayansi na Teknolojia wanafunzi hawajafanya vizuri, tulibebe jukumu hili kabla ya wanafunzi hawajafanya mtihani wao wa kumaliza elimu ya msingi Septemba mwaka huu", amesisitiza Balandya.

"Tunapaswa kuiunga mkono Serikali ya Rais Samia ambayo imeleta zaidi ya Tshs. bilioni 16 kwa  mikoa ya Kanda ya ziwa (2023/24) Mwanza ikipata shs bilioni 4.3 kwa ajili ya kuboresha elimu ukiwemo ujenzi wa shule mpya, nyumba za walimu na matundu ya vyoo," Balandya.

Akitoa taarifa fupi ya mtihani huo wa Utamilifu kwa niaba ya Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza, Afisa Taaluma Mkoa anayeshughulikia elimu ya Sekondari Aisa Rupia amesema mtihani huo umefanyika Mei 22 hadi 23 mwaka huu ikijumuisha Halmashauri 37 yenye jumla ya shule 4205 kati ya hizo 3834 za Serikali na 371 za binafsi.

"Ndugu Mwenyekiti watahiniwa wamepimwa katika masomo sita ambayo yanafundishwa kulingana na mtaala mpya ulioboreshwa ambayo ni Hisabati, Kiingereza,Kiswahili,Sayansi na Teknolojia,Maarifa ya Jamii na stadi za kazi, na Uraia na Maadili,"Rupia

Wakati huo huo Elikana, leo asubuhi Ofisini kwake amekutana na uongozi wa Shirika linalowasaidia watoto wa kike elimu ya stadi za maisha kuanzia kidato cha kwanza, CAMFED TANZANIA ambao watafanya shughuli hiyo kwenye wilaya za Magu, Misungwi, Kwimba na Halmashauri ya Buchosa.

Katika mazungumzo mafupi mtendaji huyo wa Mkoa ameutaka ujumbe huo ambao ni walimu kitaaluma kuweka mkazo wanafunzi kuyapenda na kuyachangamkia masomo ya Hisabati na Sayansi.

Kiongozi wa kundi hilo Mussa Siame amesema mwaka huu wamepangiwa maeneo hayo na changamoto watakazo zibaini wataziwasilisha Tamisemi.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti