RAS BALANDYA LEO ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KIFO CHA HAYATI ALI HASSAN MWINYI
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana leo Machi 05, 2024 amesaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia tarehe: 29 Februari 2024, Dar es Salaam na kuzikwa tarehe: 02 Machi 2024, Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini, Unguja.

