• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RAS MWANZA ATOA RAI KWA WARATIBU TASAF KUTUMIA MFUMO WA MANUNUZI KWA UFANISI

Posted on: February 21st, 2024

RAS MWANZA ATOA RAI KWA WARATIBU TASAF KUTUMIA MFUMO WA MANUNUZI KWA UFANISI


*Aagiza kutatuliwa kwa changamoto zote ili Mfumo wa NEST utumike ipasavyo*


*Atoa wito kwa Maafisa hao kutoa taarifa za uaminifu kwa walengwa kwa wakati*


*Asema Mwanza imepokea zaidi ya Bilioni 91 kuanzia Julai 2015 kwa wanufaika*


*Ataka wafuatiliaji kuwa wazalendo katika kuwafikia walengwa na wanufaika*


*Asema zaidi ya miradi 174 ya zaidi ya Bilioni 33 imetekelezwa Mwanza*


Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana amewataka Waratibu na watendaji kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) kuzingatia Sheria na Kanuni za Matumizi ya Mfumo wa Manunuzi (NEST) na Utoaji wa taarifa ili kuwahudumia walengwa kwa ufanisi.

Balandya amebainisha hayo mapema leo Februari 21, 2024 wakati akifungua Kikao kazi cha kujadili maendeleo ya Utekelezaji wa Mpango wa TASAF na Matumizi ya Mfumo wa Manunuzi (NEST) na Mfumo wa Taarifa wa TASAF kinachofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

"Mfumo wa Ununuzi na Mfumo wa Utoaji taarifa wa TASAFni muhimu sana katika Utekelezaji wa Mradi wa TASAF kwa ujumla wake katika kuhakikisha umasikini unaondoka kwa wananchi  kama ilivyokusudiwa na wafadhili wa mradi huo." Amesema Katibu Tawala.

Aidha, Katibu Tawala huyo amebainisha kuwa Mwanza imepokea zaidi ya Bilioni 91 kuanzia Julai 2015 kwa wanufaika 71,381 huku zaidi ya miradi 174 ya zaidi ya Bilioni 33 ikitekelezwa Mkoani humo tangia uzinduzi rasmi wa mradi huo Mkoani Mwanza mpaka sasa na kwamba fedha hizo ni nyingi zinahitaji uzalendo kwenye usimamizi.

Bi. Haika Shayo, Mkurugenzi wa Uratibu kutoka TASAF amesema wapo Mwanza katika kikao kazi cha kawaida cha kupitia utekelezaji wa shughuli za mradi  ili kuhakikisha mradi huo unafanyika kwa ufanisi na kujifunza matumizi ya Mfumo wa Ununuzi katika ngazi ya Halmashauri na Mfumo wa Taarifa wa TASAF.

"Hatuna budi kuwa na taarifa sahihi na za wakati kwa walengwa ili kuhakikisha wanaufurahia na unawahudumia kwa ufanisi hivyo baada ya kikao kazi hiki tunatarajia ufanisi mkubwa zaidi kwa watendaji wetu." Amesema Bi. Shayo, Mkurugenzi wa Uratibu TASAF.

Vilevile, amebainisha kuwepo kwa changamoto ya matumizi ya mfumo wa manunuzi hivyo ni imani yake kwamba kupitia mafunzo hayo ya siku 3 ya uwezeshaji  changamoto hiyo itatatuliwa  kwani wahusika wote ikiwemo Waratibu, Wahasibu, Maafisa Ufuatiliaji wa Mpango wa TASAF,  Maafisa Manunuzi  wamehusishwa katika mafunzo haya.

Monica Mahundi, Mratibu wa Mpango wa TASAF Mkoa wa Mwanza amebainisha kuwa jumla ya wanufaika 71,381 wamefikiwa huku Miradi 174 katika Sekta za Elimu, Afya na Miundombinu ya Barabara yenye zaidi ya Bilioni 33 zimepokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti