• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RAS MWANZA ATOA WITO KWA WADAU WA AFYA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUSAIDIA SEKTA HIYO

Posted on: February 7th, 2025

RAS MWANZA ATOA WITO KWA WADAU WA AFYA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUSAIDIA SEKTA HIYO


Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza ndugu Balandya Elikana ameipongeza Idara ya Afya Mkoani humo kwa ufanisi kwenye kazi kwa kushirikiana na wadau jambo linalofanya Mwanza iendelee kuwa salama wakati wote pamoja na uwepo wa hatari ya magonjwa ya mlipuko.

Ametoa pongezi hizo leo tarehe 07 februari, 2025 wakati akifungua kikao cha Wadau wa Afya kilichoketi kwenye Ukumbi mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa madhumuni ya kukumbushana wajibu katika kuhudumia jamii ili iendelee kuwa salama.

Aidha, amebainisha kuwa Mkoa wa Mwanza umejipanga kukabiliana na magonjwa ya Mlipuko kama Marburg pamoja na kuendelea kutoa huduma bora za afya kwa kushirikiana na wahisani wa ndani kutokana na kujitoa kwa baadhi ya mataifa tajiri.

Amesema, Mwanza imeshaandaa kikosi kazi cha watumishi wa afya zaidi ya 264 ambao wamepewa mafunzo maalumu ya mapambano ya ugonjwa huo na jinsi ya kumhudumia mgonjwa atakayeambukizwa na akatoa wito kwa wadau kuunga mkono juhudi hizo kwa rasilimali zozote zitakapohitajika.

Halikadhalika, ametoa wito kwa wadau kushirikiana na serikali katika kuhudumia watumishi zaidi ya 600 waliokua kwenye ufadhili wa mashirika wahisani kutoka nje ili huduma za msingi zisikwame kwa kutumia rasilimali zilizopo.

Naye, Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Dkt. Jesca Lebba amebainisha kuwa idara ya Afya mkoani humo wameamua kukutana na Wadau pamoja na mambo mengine ili kupitia maandalizi ya bajeti 2025/2026 na kuandaa mpango kazi wa mwendelezo wa kazi za afya baada ya baadhi ya wahisani wa nje kujitoa kwenye ufadhili.

Kaimu mratibu wa magonjwa ya milipuko Dkt. Gabriel Mashauri amesema Marburg ni ugonjwa wa mlipuko unaosababishwa na virusi vya Marburg na unaambukizwa kwa haraka kupitia njia ya damu, mate, mkojo, jasho, choo kikubwa, matapishi, maji ya uzazi na hata kugusana na dalili zake ni kutokwa damu mwilini.

Amefafanua kuwa wafanyakazi wa Afya wapo kwenye hatari zaidi ya kuambukizwa  na uwezekano wa kifo hutofautiana kati ya 24% hadi 88% hivyo ni ugonjwa hatari unaosababisha vifo kwa haraka hivyo basi watu wanapaswa kuelimishwa kutochangia nguo au vitu vyenye ncha kali.

Aidha, Dkt. Mashauri amezitaja dalili za mtu aliyepata na maambukizi hayo kuwa ni pamoja na  kuumwa kichwa, homa, maumivu ya misuli, mwili kuishiwa nguvu, vidonda vya koo, vipele vya ngozi, maumivu ya tumbo, kuharisha (damu), kutapika damu na kutokwa damu.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti