• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RAS Mwanza awataka Vijana kujitambua na Elimu ya Afya.

Posted on: June 8th, 2022

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike amewataka Vijana kujitambua wao ni nguvu kazi ya Taifa hivyo wasikubali kuyumbishwa na mabadiliko ya ki-Dunia ambayo baadhi yao wamejikuta yakiwagharimu maisha yao.


Katibu Tawala Ngusa amesema hayo wakati wa Mdahalo Maalum uliohusu Ukatili wa Kijinsia uliofanyika Chuo Kikuu cha Mt.Agustino Mkoani Mwanza,amesema rika la Vijana wengi kuanzia miaka 18 hadi 25 wamekumbwa na majanga ya kila aina kuanzia utumiaji wa Dawa za kulevya na Ngono isiyo salama  ambavyo kwa pamoja vimewapotezea ndoto zao za kimaisha.


"Huku vyuoni mambo mengi yasiyo na tija kwenu yanafanyika baadhi yenu mnaishi kama mke na mume,upigaji wa picha za utupu wengine kujiua,haya yote ni lazima mpambane kuyatokomeza kama mna nia njema na maisha yenu"


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha SAUT, Prof Hosea Rwegoshora amebainisha kinacho wagharimu Vijana wengi ni tamaa ya kulazimisha kufanikiwa ki-maisha bila kujali wanatumia njia gani sahihi.


Afisa Ustawi wa Jamii Mkoani Mwanza, Faith Lukindo amesema mkazo wa elimu hauna budi kuwekwa kwa Vijana kuanzia ngazi za Shule kutokana na kundi hili kuwa katika hatari zaidi na kasi ya mabadiliko ya ki-dunia.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Wadada, Lucy John amesema kwa kutambua umuhimu wa Vijana katika ujenzi wa Taifa wameamua kuwajengea msingi mzuri wa elimu ya Afya ambayo itawasaidia kupambanua baya na zuri.


Baadhi ya watoa Mada alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike,Mratibu wa Dawati la Jinsia kutoka Polisi,Faraja Mkinga, Mratibu wa Afya ya Uzazi Mwanza, Bertha Mkinga, Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa Faith Lukindo, pamoja na Mhadhiri msaidizi kutoka SAUT, Fides Zakayo.

Mdahalo huo umewashirikisha wanafunzi kutoka baadhi ya Vyuo vilivyopo Mkoani Mwanza na Makundi mengine ya Vijana.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti