• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC Malima ahimiza kilimo Bora cha Pamba Wilaya za Magu na Kwimba

Posted on: August 5th, 2022


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Adam Malima amewataka viongozi na watendaji wa Halmashauri za Wilaya ya Magu na Kwimba kutoa Elimu ya Kanuni bora za kilimo cha pamba kwa wananchi ili kuwa na ushirikishwaji wa wakulima katika maendeleo ya uzalishaji wa zao hilo.

Ameyasema hayo katika nyakati tofauti  Agosti 05, 2022 alipofika kwenye wilaya hizo kujitambulisha na kutoa dira ya maendeleo katika kuwahudumia wananchi kufuatia kuteuliwa kwake hivi karibuni na Mhe. Rais kuongoza Mkoa huo.

"Napenda kuwapongeza sana Mkurugenzi na timu yako kwa ukusanyaji wa mapato ya ndani hadi mmevuka malengo yenu lakini pamoja na hilo nawaomba tutilie Mkazo zao la pamba ambalo ndio uchumi wa wananchi na sina wasiwasi maana nimeambiwa kuwa shamba darasa la Mkoa lipo hapa" Mhe. Malima akiwa Magu.

Aidha, ametoa rai kwa RUWASA na MWAUWASA kuhakikisha wanaguswa na changamoto ya Maji kwa kila eneo ambalo wananchi wanakosa huduma hizo na amewataka kuweka nguvu kuhakikisha wanaitunza miradi ya maji ili iweze kuwahudumia wañanchi kwa muda mrefu.

Katibu Tawala wa Mkoa, Balandya Elikana amewataka watumishi kwenye Wilaya hizo kufanya kazi kwa bidii ili kuwapa wananchi huduma stahiki ili kutimiza dhima na kiu ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutaka kuona wananchi wake wanaendelea kiuchumi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe. Salum Kali amemhakikishia kiongozi huyo ushirikiano wa dhati na amebainisha kuwa viongozi ndani ya wilaya hiyo wana ushirikiano wa dhati ambao umezaa Matunda ya kuongoza kwa Ukusanyaji wa Mapato ya ndani kwa Mkoa wa Mwanza.

"Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ametuletea fedha nyingi sana za kutekeleza miradi mingi kwenye kila sekta na tunayo miradi ya kimkakati, tunajengewa hadi shule kubwa ya kisasa kwa Tshs. Bilioni 4 na itakua na uwezo wa kuchukua zaidi ya wanafunzi elfu moja na ukienda kwenye Afya miradi inaendelea." Mhe. Kali.

"Halmashauri ya wilaya ya Kwimba ilikasimia kukusanya Tshs Bilioni 2.4 kwa mwaka wa fedha uliopita na hadi kufikia Juni 30, 2022 tumefanikiwa kukusanya Tshs Bilioni 2.9 sawa na 106% na kwa 2022/23 Halmashauri inakusudia kukusanya Tshs Bilioni 3.1 na tunayo mikakati mbalimbali ya kufikia lengo tulilojiwekea na hata kuvuka lengo." Mkuu wa Wilaya Kwimba.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti