• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MAKALLA AHIMIZA USHIRIKIANO KATIKA KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI

Posted on: May 31st, 2023

*RC MAKALLA AHIMIZA USHIRIKIANO KATIKA KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI*


*Aahidi kusimamia suala la Usalama kwa wananchi*


*Awataka Watumishi kuwa na nidhamu kazini, kutoa huduma bora*


*Ataka kuondoshwa kwa hoja za Ukaguzi na kutatua changamoto za ardhi*


*Awaagiza Sekta ya Maji kutatua kero ya upatikanaji wa huduma hiyo*


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos Makalla ametoa rai kwa Viongozi na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kushirikiana naye kwa dhati ili kutoa huduma bora na kuwaletea maendeleo wananchi.

Mhe. Makalla amesema hayo mapema leo Mei 31, 2023 wilayani Nyamagana wakati akizungumza na Viongozi, watendaji na  Makundi mbalimbali yakiwemo ya wanasiasa, wafanyabiashara na kamati ya Amani ya Wilaya hiyo kwa lengo la kujitambulisha rasmi.

Amesema ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ni lazima watendaji na viongozi waliopewa dhamana ya kuhudumia wananchi kushirikiana kwa dhati na kufanya kazi kwa weledi ili kuwatatulia kero zao za kila siku wananchi.

Aidha, ameagiza ngazi zote za uongozi kuanzia ofisi za wenyeviti wa mitaa kusimamia suala la usalama wa wananchi wao ili kuwe na amani na kujenga ari ya kufanya kazi katika nyanja mbalimbali kwenye maeneo yao ikiwemo uvuvi, kilimo na biashara.

"Ipende kazi yako, fanya kazi kwa bidii, toa huduma bora kwa jamii na tukiwahudumia vema wananchi watakua na furaha kwani matatizo yao yatasililizwa na watahudumiwa vizuri, tukumbuke kuwa mwananchi akikosa huduma atailalamikia ofisi na sio wewe uliyemkwamisha kwa kujua tu haki bila wajibu." CPA Makalla akisisitiza juu ya uwajibikaji.

Vilevile, ameagiza Watumishi kujibu hoja za ukaguzi kwa wakati ili kuleta imani kwa wananchi na kwamba idara ya ardhi kujipanga kutimiza wajibu kwa kuzingatia matumizi bora ya ardhi na kutatua changamoto za ardhi kwa wananchi ili kuwa na mji uliopangiliwa vizuri.

"Moja ya maswali magumu ya Wananchi ni kwamba kwanini Mwanza iwe na shida ya Maji wakati ziwa lipo hapa jirani na huku wakiangalia Shinyanga wanapata maji kutoka hapa hivyo tuzuie upotevu wa maji kwani hiyo ni moja ya sifa mbaya sana kwahiyo lazima tuwe na mipango ya kutatua shida ya Maji kwa wananchi." Mhe. Makalla.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi amesema kwa mwaka 2022/23 Halmashauri hiyo imekadiria kukusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 23.6 na hadi  Aprili 2023 wamekusanya kwa ziaidi ya asilimia 75 ambapo ni ongezeko kubwa lilichagizwa na mipango kazi kabambe waliyojiwekea ukiwemo upangaji wa Wafanyabiashara kwenye maeneo rasmi.

Vilevile, amefafanua kuwa kutokana na mikakati waliyojiwekea ikiwemo kuwa na timu maalum ya Ukusanyaji wa mapato hadi kufikia mwishoni mwa  Juni mwaka huu Halmashauri ya jiji la Mwanza wanakusudia kufikia lengo na hata kuvuka ili kufanya vizuri kama mwaka uliopita ambao walikusanya Mapato ya ndani ya zaidi ya asilimia 105.

Aidha, Mhe. Makilagi amebainisha kuwa wamepokea fedha za Miradi ya Maendeleo kwa asilimia 77 kwani zaidi ya Shilingi Bilioni 79 zimepokelewa na kwa upande wa miradi ya kimkakati kama Meli ya MV Mwanza Bilioni 109, Ukarabati wa Meli ya MV Umoja  Bilioni 19 Stendi ya Mabasi ya Nyegezi Bilioni 18 na Soko kuu la Kisasa Bilioni 17 yote inaendelea vizuri kwani wakandarasi hawadai fedha na yote ipo hatua za ukamilishaji.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti