• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MAKALLA AIKABIDHI RASMI HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA TIMU YA SOKA YA PAMBA FC

Posted on: July 14th, 2023

*RC MAKALLA AIKABIDHI RASMI HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA TIMU YA SOKA YA PAMBA FC*


 *Asema kipaumbele chake ni Mwanza kuwa na timu ya Ligi Kuu**


 **Mwanza ina vipaji vya soka,viwanja vizuri vya mpira na Chuo cha michezo Malya.*


*Uendeshaji Michezo inahitaji fedha pia michezo inachochea uchumi na Utalii wa michezo.*


 *Awaomba wananchi Mkoa wa Mwanza kuwa Na Umoja*


Halmashauri ya Jiji la Mwanza leo Julai 14,2023 inatarajia kupokea barua rasmi ya kukabidhiwa na kuiendesha  timu ya soka ya Pamba FC maarufu kama TP LINDANDA kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza baada ya mchakato wa umiliki kutoka bodi ya Pamba na kuletwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kukamilika.

Akizungumza leo na wadau wa michezo kwenye ukumbi mkubwa wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA Amos Makalla amebainisha Mkoa huo una kila sababu ya kuwa na timu ya Ligi kuu kutokana na historia yake nzuri ya kuwa na vipaji vya soka na miundombinu bora ya viwanja.

Amesema baada ya kukabidhiwa rasmi timu ya Pamba kwa barua alikutana na uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza chini ya Mkurugenzi Aaron Kalugumjuli na kuwauzia wazo la kuimiliki na kuiendesha na walikubali kwa mikono miwili,hivyo leo baada ya kikao hicho atamkabidhi naye rasmi kwa barua.

"Ndugu zangu nimewaita hapa wengi wenu mnajua mimi ni mdau kindaki ndaki wa soka nikianzia kuucheza kwa muda mrefu katika mpira wa kisasa huwezi kufanikiwa kwa vimichango vidogo vidogo ni lazima sasa tuingie katika sura mpya sitakuwa nautendea haki Mkoa huu kama tutakosa timu ya Ligi Kuu",amesisitiza CPA Makalla.

Katika Mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi wa Chama cha Soka Mwanza na uongozi wa timu ya Pamba,Mkuu huyo wa Mkoa amehimiza mchakato wa kuundwa kamati ya mpito kwa lengo la kukamilisha hatua zote muhimu za usajili na mapendekezo ya kocha wachezaji gani wabaki na nani wakuwachwa yafanyike haraka.

" Tuutumie muda huu mchache vizuri kuanzia marekebisho ya benchi la ufundi,na tuangaze baadhi ya wachezaji bora wa Ligi kuu waje kuchanganyika na hawa ili tupate timu imara itakayo kuja kuutoa kimaso maso Mkoa wa Mwanza," amehimiza Mkuu huyo wa Mkoa.

"Sisi kama viongozi wa soka Mkoani hapa,hatua hii imetufariji na mwanga wa kucheza Ligi kuu tunauona, hasa ikizingatiwa kuendesha timu kwa mafanikio kuna hitaji fedha nyingi," Vedasto Lufano,M/kiti MZFA.

"Hadi leo tulikuwa tumejichangisha Shs Milioni 14 kwa ajili ya kuiendesha timu msimu huu,lakini kwa taarifa hii timu ya kuwa chini ya Halmashauri ni dhahiri tutafika mbali,tunakushukuru mno Mhe. Makalla,"Evaristi Hagilla,M/kiti Klabu ya Pamba

Kwa zaidi ya miaka 20 timu ya soka ya Pamba haijashiriki Ligi Kuu licha ya kutamba miaka ya 90 na kutoa wachezaji wengi waliong'ara kwenye vilabu vikubwa vya Simba na Yanga akiwemo George Masatu.Hussein Marsha,John Makelele na Fumo Felician.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti