• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MAKALLA AKIPONGEZA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA KUJENGA CHUO CHAKE MWANZA

Posted on: December 7th, 2023

RC MAKALLA AKIPONGEZA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA KUJENGA CHUO CHAKE MWANZA


*Aahidi uwepo wa maji ya kutosha kwenye eneo lake la ujenzi baada ya Mradi Mkubwa wa maji kukamilika*


*Akitaka chuo kuipa kipaumbele Mwanza kutokana na kukua kiuchumi*


*Wahitimu watakiwa kuwa wabunifu kupitia taaluma yao kujiajiri wenyewe*


*Atangaza fursa za kiuchumi Mwanza mara baada ya miradi ya kimkakati kumalizika*


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA Amos Makalla amekipongeza Chuo cha usimamizi wa fedha IFM kwa hatua ya kujenga chuo chake  na kuahidi changamoto ya maji eneo la ujenzi itamalizika hivi karibuni kutokana na mradi wa maji Butimba kukamilika.

Akizungumza leo na wahitimu wa ngazi mbalimbali katika mahafali ya 49 ya Chuo cha usimamizi wa fedha IFM kampasi ya Mwanza na Simiyu yaliyofanyika ukumbi wa Rock City Mall, Mkuu huyo wa Mkoa amesema chuo hicho kuwa na majengo yake sasa itakuwa na wigo mpana wa kuwachukua wanafunzi wengi na hasa mahitaji makubwa ya wataalamu wanaohitajika Mkoani humo.

"Ndugu Mwenyekiti wa Baraza la uongozi Prof. Emmanuel Mjema, Mkoa wa Mwanza una miradi mingi ya kimkakati na unachangia kwa kiasi kikubwa pato la Taifa,hivyo wataalamu bora kwa upande wa fedha na uchumi watahitajika kutoka Chuoni kwako," CPA Makalla.

Aidha, amewataka wahitimu hao kwenda mtaani kuwa chachu ya mageuzi ya kiuchumi ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla na siyo vyeti hivyo kwenda kuvifungia kabatini.

"Ni lazima tutambue mara baada ya kutoka hapa suala la ajira bado ni changamoto, hivyo miende mkawe wabunifu wa kujiajiri wenyewe na hasa fursa nyingi za kiuchumi zilizopo Mkoani Mwanza kuanzia Utalii na uchumi wa bluu,"amefafanua Mkuu huyo wa Mkoa wakati anazungumza na wahitimu hao.

CPA Makalla amesema Mkoa wa Mwanza umejaliwa miradi mingi ya kimkakati kuanzia mradi wa reli ya kisasa SGR, Daraja la JP  Magufuli,u uenzi wa Meli ya Mv Mwanza pamoja na ujenzi wa uwanja wa ndege wa kisasa, miradi yote hiyo itakapo kamilika itahitaji wataalamu na pia fursa za kujiajiri zitakuwepo kwa wingi.

"Ndugu mgeni rasmi Chuo chetu cha IFM kimezidi kupiga hatua na sasa tuna jumla ya kampasi tatu Mwanza,Dodoma na Simiyu na sasa tupo mbioni kufungua kampasi ya nne huko Mkoani Geita,lengo ni kutoa wataalamu bora hapa nchini," Prof.Emmanuel Mjema,M/kiti wa Baraza la uongozi chuo cha usimamizi wa fedha IFM

Akizungumzia maendeleo ya Chuo hicho Mkuu wa chuo cha IFM Prof. Josephat Mtoto amebainisha walianza na wanafunzi 72 mwaka 1992 na sasa wamepiga hatua kwani mwaka 2022-23 wamekuwa na jumla ya wanafunzi 15,000.

Jumla ya wahitimu 564 wamehitimu masomo yao ya ngazi mbalimbali kuanzia astashahada,shahada na shahada ya uzamili.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti