• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MAKALLA APINGA MKANDARASI MAJI BUTIMBA KUONGEZEWA MUDA BILA KULIPA FIDIA

Posted on: August 3rd, 2023


- Adai mamlaka na Wizara kumuongezea muda bila fidia  ni kinyume vha utaratibu na sheria

- Serikali mara zote imehaidi kwa wananchi mradi utakamilika Julai 31,2023

- Ataka mkandarasi akatwe fedha za fidia zaidi ya Bilioni 2 ili iwe fundisho.


Mkandarasi anayetekeleza  mradi mkubwa wa maji wa Butimba,Kampuni ya Sogea Satom kutoka Ufaransa ametakiwa kulipa adhabu ya kisheria ya malipo ya Shs bilioni 2.5 kutokana na kuzembea kukamilisha mradi huo kwa wakati na badala yake kuongeza muda kinyemela bila uongozi wa Mkoa kujulishwa.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA Amos Makalla ametoa agizo hilo leo ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa wakati wa ziara yake miezi michache iliyopita na kuahidiwa mradi huo kukamilika Julai 31,2023,amesema kitendo cha kuongezewa Mkandarasi miezi mitatu kinyemela ikiwa ni mara ya pili hakikubaliki na ni kwenda kinyume na maagizo ya Rais Samia Suluhu aliyetaka mradi huo kukamilika kwa wakati.

"Hiki kitendo narudia kusema hakikubaliki,ni lazima Mkandarasi huyu akatwe hiyo fidia ili naye fedha hizo zimuume kwani ni dhahiri hatambui wananchi wa Mwanza wanavyotaabika na kukosa huduma hiyo

 kwa muda mrefu",amesema CPA Makalla.

Ameiagiza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji Mwanza,MWAUWASA kukaa na Wizara ya maji kuanza kutekeleza mara moja kumkata fedha hizo kwa muda huo wa miezi mitatu ili iwe fundisho kwa Wakandarasi  wengine wababaishaji.

"Hili jambo linashangaza sana Mkandarasi amelipwa fedha kwa asilimia 100 mimi nawahaidi wananchi kuanza kupata huduma ya maji ya uhakika kuanzia Julai 31 baada ya kuongezewa muda Februari mwaka huu,huyu Mkandarasi hana sababu yoyote ya kuongezewa muda lakini sasa ni lazima amalizie hiyo miezi 3 pamoja na adhabu hiyo malipo ya fedha kwa kweli sijaridhika kabisa ,"CPA Makalla.

"Mhe.Mkuu wa Mkoa sisi kama MWAUWASA tunakuahidi kuanzia Septemba 15 wananchi wa Mwanza wataanza kupata maji wakati Mkandarasi atakapoanza zoezi la majaribio,hivyo tunaamini changamoto ya ukosefu wa maji kwa wananchi itakwisha,"Mhandisi Robert Lupoja,Kaimu Mkurugenzi MWAUWASA.

Kampuni ya Sogea Satom imeanza kutekeleza mradi huo wa maji Butimba wenye gharama ya Shs bilioni 70 kuanzia mwaka 2021 huku uzalishaji wa maji kwa Mkoa wa Mwanza ukiwa ni lita milioni 90 kwa siku na mahitaji halisi ni lita milioni 160 kwa siku na kukiwa na upungufu wa zaidi ya lita milioni 60.






Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti