• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MAKALLA AWAHAKIKISHIA USHIRIKIANO WAANDISHI WA HABARI MWANZA

Posted on: February 23rd, 2024

RC MAKALLA AWAHAKIKISHIA USHIRIKIANO WAANDISHI WA HABARI MWANZA


*Amewashukuru Waandishi kwa kutumia vema kalamu zao kuunganisha jamii*


*Aelekeza Taasisi zote Mwanza kutoa ushirikiano kwa wanahabari*


*Awaasa wanahabari kuandika kutoka kwenye vyanzo vya uhakika na ukweli*


*Abainisha ujenzi wa Jengo la Abiria la kisasa Airport Mwanza kuwa Kimataifa*


*Aahidi usaidizi  wa Pikipiki 2 na kuongoza Harambee ya ujenzi wa ofisi*


*Awasihi kutangaza miradi ya kimkakati na timu za Mwanza kucheza Ligi kuu*


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla amesema Ofisi yake itaendelea kushirikiana na waandishi wa habari kwenye kuhabarisha umma na kuhakikisha jamii inapata taarifa sahihi kwa wakati na kwa uhakika.


Makalla amesema hayo leo Februari 23, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa huo kupitia chama chao (MPC)  katika kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Makalla ametumia wasaa huo kubainisha furaha yake kwa waandishi wa habari hao kwani wamekua kiungo cha kuwafikia wananchi na ameomba umoja udumishwe zaidi kwenye ofisi mbalimbali ili kuifanya Mwanza kukua zaidi kiuchumi na maendeleo ya huduma za Jamii.


Aidha, amebainisha mpango wa Serikali wa kuboresha uwanja wa Ndege wa Mwanza kuwa wa Kimataifa hususani ujenzi wa Jengo la abiria la kisasa litakaloanza kujengwa ndani ya wiki mbili zijazo na kwamba utasaidia kukuza utalii mkoani humo.

Mwenyekiti wa MPC Edwin Soko ametumia wasaa huo kuwasilisha ombi kwa Mkuu wa Mkoa kuwa mgeni rasmi kwenye Harambee ya Kuchangia fedha za ujenzi wa Ofisi ya Chama hicho itakayofanyika siku za usoni.

Aidha, Soko amebainisha kuwa waandishi wa habari mkoani humo wapo kwa ajili ya kuhabarisha umma na kusaidia kupatikana kwa majawabu ya changamoto mbalimbi kwa jamii jambo ambalo wanafanya kwa weledi na kuzingatia maadili ya uandishi.

"Tunafanya kazi zetu kwa kuzingatia weledi na maadili hususani kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2025" Amesema Mwenyekiti Soko.


Vilevile, ametumia wasaa huo kuziomba taasisi na mamlaka zote za Serikali Mkoani humo kuhakikisha wanazingatia usalama wa waandishi wa habari wakati wote wanapotumikia shughuli za uhabarishaji wa umma na kutowazungusha waandishi mara wanapohitaji taarifa.

Katika kuhakikisha wanakua na Ofisi yao na kuondokana na gharama za kupanga,  Soko ametoa rai kwa Mkuu wa Mkoa kuwasaidia waandishi wa Habari kwenye upatikanaji wa vitendea kazi mbalimbali vya Studio na vinginevyo pale ambapo Makalla ameridhia na kuahidi kuwanunulia Pikipiki 2 siku za usoni.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti