• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC Malima ahimiza ushirikiano wa kimaendeleo na viongozi wa Kimila Mwanza

Posted on: May 11th, 2023

*RC Malima ahimiza ushirikiano wa kimaendeleo na viongozi wa Kimila Mwanza


Viongozi wa Kimila wa Mkoani Mwanza wameombwa kuushirikisha uongozi wa Mkoa  katika kazi zao pamoja na mambo ambayo yakipata ushirikiano wa Uongozi yanaweza kuleta maendeleo katika Mkoa huo.

Wito huo umetolewa leo Mei 11, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima wakati alipokutana na Viongozi wa Kimila wa Mkoani humo katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

" Kama yapo mambo ambayo yanahusiana na mafanikio katika kazi zenu basi naomba mnishirikishe  hata katika mambo yote ambayo yanaweza kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa watu wa Mwanza na kanda ya Ziwa kwa ujumla," RC Malima

Aidha Mhe. Malima ameongeza kuwa  serikali ya Mkoa kwa kushirikiana na Chuo cha Mt. Augustino (SAUT) wanampango wa kuanzisha (Kituo cha Ubunifu cha Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia) ili kiweze kuwasadia  wananchi wa Mkoa huo.

 Serikali ya  Mkoa  imeamua kufanya kampeni mahususi  ili kujaribu kuwafikia wananchi wake kwahiyo kuna kituo cha kuhamasisha maendeleo ya kiuchumi( Kituo cha Ubunifu cha Maendeleo na Sayansi na Teknolojia) ambacho tunataka tukianzishe kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Mt. Augustino (SAUT)," Amesema Mkuu huyo wa Mkoa

Naye Mtemi. Charles Itale wa kwanza wa  Bujashi Magu na  Mwenyekiti wa Umoja wa Watemi Mkoa wa Mwanza  ameongeza kiwa kitu kinachosababisha mmomonyoko wa maadili ni kuchukulia swala la malezi kama jukumu la mtu mmoja na sio la jamii kwa ujumla jambo ambalo linaleta utofauti na zamani

Pia  Mtemi. Domina Musiba wa Tatu wa Buchosa amewaomba viongozi wa kiserikali na wa kidini waweze kusimamia maswala ya kimaadili na pia wapate wasaa wa kuielimisha jamii pale wanapokutana nayo ili waweze kurudisha maadili kama kipindi cha zamani

"Tunaomba sana viongozi wote wa dini hata wa Serikali  wanapokutana na wananchi waweze kusimama na kutoa elimu kuhusu mambo ya maadili kwa jamii na  pia wajenge uhusiano mzuri na Watemi ili tuweze kukutane na  kuuzungumza kuhusu maadili na mienendo ya jamii zetu kwa ujumla.

Mkutano huo wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na viongozi wa kimila ulilenga kujadili maswala ya mmomonyoko wa maadili katika jamii na kujadili juu ya tamasha la bulabo ambalo ni maalum kwa ajili ya  kusherehekea mavuno kwa mila za kabila la Kisukuma ambazo zitafanyika Juni 11 hadi 17 2023 katika kata ya  kisesa wilaya ya Magu.


Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti