• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC Malima apokea mtambo wa kuchimba Visima,aishukuru Serikali ya Rais Samia

Posted on: March 3rd, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima amekabidhiwa mtambo wa kisasa wa kuchimba Visima na Malambo yenye thamani ya Shs milioni 550 ambayo itaanza kuchimba Visima 83 kwenye baadhi ya maeneo Mkoani humo.

Akizungumza katika hafla fupi ya kuwakabidhi mitambo hiyo kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) iliyofanyika Wilayani Misungwi, Mhe.Malima amesema licha ya Mkoa wa Mwanza kuwa na rasilimali kubwa ya maji ya Ziwa Victoria lakini kuna baadhi ya maeneo wananchi hawapati huduma hiyo hivyo mtambo huo ni ukombozi wa kumtua ndoo kichwani mwanamke.

"Kwa niaba ya wananchi wa Mwanza natoa shukran kwa Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ameonesha upendo wa dhati wa kuendelea kuwapigania maendeleo wananchi wake,nawaomba sana tuitunze na tuitumie kwa malengo yaliyokusudiwa mitambo hii".Amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.

"Mhe.Mkuu wa Mkoa bado tunaendelea kupambana kuhakikisha huduma ya maji vijijini  tunafikia asilimia 85 na mijini 95 hadi kufika mwaka 2025 kwa mujibu wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi inavyotutaka".Mhandisi Godfrey Sanga.Meneja RUWASA Mkoa

Amesema uchimbaji wa Visima 83 kwa bei ya Mkandarasi ingefikia Shs.2,554,265,406 lakini kwa kutumia mitambo hii  wanatarajia kutumia Shs.2,118,575,000 hivyo wameokoa Shs.435,690,406.

Mitambo hiyo ya kuchimba Visima imesambazwa Mikoa yote 25 ya Tanzania Bara iliyogharimu zaidi ya Shs Bilioni 15.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa akiwa njiani kwenda kukagua miradi ya maji huko Ihelele Wilayani Misungwi amepita kwenye shamba la Uzalishaji Mifugo la Mabuki na kutoa maelekezo kwa Maafisa Mifugo wote kutoka Halmashauri kukutana kwa ajili ya kuweka mkakati wa kujifunza namna ya ufugaji wenye tija wa kuwa na Mifugo michache yenye ubora na kumuingizia kipato mkulima.

"Nimepita hapa nami kuna somo nimelipata ambalo ni lazima wasaidizi wangu waje hapa kujifunza ili wakamsaidie mfugaji namna ya kujiongezea kipato kwa ufugaji wa kisasa".Amesema Mhe.Malima.

"Shule hii ya Sekondari ya wasichana ya Mwanangwa inayojengwa na TASAF, naendelea kusisitiza Miradi hii yote iwe imekamilika mwishoni mwa Machi mwaka huu kama tulivyoahidi kwa Waziri Mhagama kuwa tutamaliza Miradi yote ya TASAF kabla ya Aprili hasa baada ya kuonesha kuwa nyuma kukamilisha Miradi mingi licha ya fedha kutolewa zote na kuwa hatarini Mkoa wetu kukosa fedha nyingine awamu ijayo ya TASAF" Amehimiza Mhe. Malima alipopita kukagua shule hiyo itakayoanza Januari mwakani.

TASAF imetoa jumla ya Shs milioni 683,005,234.74 kukamilisha mradi wa shule hiyo.

Akiwa kata ya Nyamahiza kusikiliza kero za Wananchi, Mkuu huyo wa Mkoa ameiagiza  RUWASA na TANESCO kuwaharakishia Maendeleo wananchi kwa kuwaletea huduma haraka na kuwataka walimu wa shule ya Sekondari Magufuli kufuata taratibu za Utumishi wa umma baada ya kupata taarifa za kuwepo upungufu wa walimu ambao wameondoka huku wakitoa visingizio visivyo na tija.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti