• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC Malima awaaga Pamba FC,awataka watimize ndoto yake kuiona ikicheza Ligi Kuu ya NBC

Posted on: May 16th, 2023

*RC Malima awaaga wachezaji wa Pamba FC, awaasa kutokata tamaa*


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro aliyehamishiwa akitokea Mwanza, Mhe. Adam Malima amewaaga wachezaji wa timu ya soka ya Pamba FC iliyopo ligi ya Championship na kuwataka kutokata tamaa katika michezo yao ijayo ya Mchujo kuwania kucheza ligi kuu ya NBC kwa msimu ujao.

Akizungumza na wachezaji na viongozi wa timu hiyo leo kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mhe. Malima amesema anaamini bado Pamba ni timu bora yenye uwezo wa kucheza Ligi kuu cha msingi ni wachezaji waongeze bidii.

"Sina shaka na nyie nimewaona uwezo wenu uwanjani, naamini dawati lenu la ufundi litafanya mkazo eneo la umaliziaji ili muweze kufunga mabao mengi,"amesema Mhe.Malima.

Malima amewasihi kushinda mchezo ujao wa mchujo dhidi ya Mashujaa FC utakaopigwa kwenye Dimba la Lake Tanganyika Mei 21, 2023 Mkoani Kigoma ili kurahisisha kazi mpambano wa marudiano utakaorindima uwanja wa Nyamagana Mei 28 2023.

Aidha, katika hafla hiyo Mkuu huyo mpya wa Mkoa wa Morogoro amewakabidhi wachezaji jumla ya Shilingi Milioni 3 ahadi yake ya fedha Shs Milioni moja pamoja na fedha kutoka kwa mdhamini wao Kampuni ya vinywaji baridi ya Jambo Shs Milioni 2.

Akitoa neno la shukrani kwa moyo aliouonesha kwa kuipambania timu hiyo Mwenyekiti wa Chama cha soka Mkoani Mwanza MZFA,Vedasto Lufano amesema wataendelea kumkumbuka Mhe. Malima kwa vitendo  kuhakikisha wanafikia malengo yao ya kucheza ligi kuu ya NBC.

"Hatuna namna yoyote ya kukufurahisha zaidi ya kutimiza ndoto zako ukiwa hapa Mkoani Mwanza kuiona Pamba FC ikicheza Ligi kuu ya NBC, hilo nakuahidi tunalipambania". Lufano

Nahodha wa Pamba FC, Jerryson Tegete amesema licha ya kukosa nafasi ya kufuzu moja kwa moja na badala yake wameingia mchezo wa mchujo wamejipanga kuwapa faraja wana Mwanza kuiona timu hiyo ikicheza Ligi kuu.

"Mhe.Malima kwa ari uliyotupa licha ya kuhamishiwa Morogoro hii ndoto yako ya kuiona Pamba FC inacheza Ligi kuu, kwa niaba ya wenzangu tunakuahidi kuitimiza," Tegete.

Pamba FC imemaliza michuano ya Ligi ya Championship msimu huu ikiwa nafasi ya tatu na mtaji wa pointi 59,hivyo kwa kanuni za TFF italazimika kucheza mchezo wa mchujo na Mashujaa FC waliomaliza wakiwa nafasi ya nne na point 49 na mshindi wa jumla atamsubiri kumenyana na timu kutoka Ligi kuu ya NBC.

Timu ya soka ya Pamba FC maarufu kama TP LINDANDA, mara ya mwisho kucheza Ligi kuu ilikuwa msimu wa mwaka 2000-2001.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti