• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC Malima awakumbusha Viongozi wa Dini kuliombea Taifa Amani,kuliepusha na Maradhi

Posted on: October 6th, 2022

*RC Malima awaomba Viongozi wa Dini kuendelea kuliombea Taifa amani, kuepukana na Maradhi*


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima amewaomba Viongozi wa Kanisa la KKKT kuendelea kuisadia Serikali katika kuboresha hali za Kiuchumi na za Watanzania kwa ujumla kupitia huduma yao ya Lutheran Mission Corporation (LMC) ambayo lengo lake ni kuratibisha kazi za Umoja za KKKT.

Mhe.Malima ameyasema hayo leo Oktoba 6,2022 alipokuwa akihutubia mkutano wa Majumuisho wa Vyama 13 vya Kimisioni vya kanisa la Kiinjili la Kilutheli kutoka Nchi za Ulaya na Marekani ambapo Tanzania ni sehemu ya waliounda Shirikisho hilo la LMC uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Isamilo Jijini Mwanza.

Ameongeza kuwa, KKKT inaweza kushiriki katika kuwawezesha waumini kuunda vikundi mbalimbali vya uzalishaji na kuvisaidia kupata mitaji,kuwa na uongozi bora na kupata elimu ya biashara.

"Wahimizeni kufanya kazi kwa bidii na kwa maarifa wakati wote, wote mnakumbuka kuwa biblia Takatifu kwenye kitabu cha Wathesalonike: 3.10 inatueleza kuwa ikiwa mtu hataki kufanya kazi basi na asile,ni imani yangu kuwa waumini mmoja mmoja au katika vikundi wakiwa na nguvu kiuchumi, kanisa litakuwa na nguvu kiuchumi na vivyo hivyo kwa Serikali," amesema Mhe.Malima.

"Ninaamini kuwa viongozi wa dini mna mchango wenu mkubwa sana katika kuishauri Serikali na kueneza amani katika nchi yetu," ameongeza.

Aidha,Amesiaitiza kuwa, KKKT imeendelea kuwajenga na kuwasadia watanzania kiroho na kimwili kwa kuwawezesha kupata maji safi na salama, elimu na huduma za afya.

Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania Mhe. Dkt. Frederick Shoo amesema anaishukuru Serikali kwa ushirikiano mkubwa kwa kanisa, kwani wamekuwa mchango mkubwa hasa katika madhehebu ya Dini ikiwa ni pamoja na KKKT.

"Mhe Mkuu wa Mkoa kwa kukubali kutenga muda wako katika ratiba iliyonayo kwako wewe kutenga muda wako kwa ajili yetu hakika ni heshima kubwa kwa kanisa letu, "amesema baba Askofu Mkuu Shoo.

Wakati akihitimisha hotuba yake Mhe.Malima amegusia Swala la Mripuko wa Ugonjwa wa Ebola uliotokea Nchi ya Jirani ya Uganda na kusisitiza kuwa mbali na kuchukua tahadhari zote ni lazima Swala la kumshirikisha na  kumuomba Mungu ni la msingi sana pia kuendelea kutoa Elimu maeneo ya ibada ili kuendelea kuchukua Tahadhari.

"Tunaomba muiunge mkono Serikali yenu na muiwezeshe kufanya kazi hiyo, tunaomba ushirikiano wakati wote na tunaomba muendelee kumuombea Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan na kuiombea Serikali kwa ujumla katika sala zenu za kila siku ili iweze kutuongoza kwa haki na kuwaletea Watanzania wote Maendeleo, kwa maana imeandikwa kwenye kitabu cha Mithali: 29.2 kuwa,Wenye haki wakiwa na amri,watu kufurahi, bali mwovu atawalapo,watu huugua, amesisitiza.

Naye Katibu Mkuu KKKT Mhandisi Robert Kitundu akimshukuru Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa, anamshukuru sana kwa kuwatia moyo kwani kwa Mhe.Malima kufika na  kusema maneno hayo wamejawa na Neema tele na kumuahidi kuwa yeye na wana KKKT wote watabaki wakimuombea.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti