• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC Malima kupanda miti milioni 3 Mwanza kukabiliana na upungufu wa uoto wa asili

Posted on: October 7th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima amesema yupo katika mkakati kamambe wa kupanda jumla ya miche ya miti milioni 3  Mkoani humo ili kukabiliana na tishio la ukame na kupungua kwa uoto wa asili.

Akizungumza leo na Viongozi na wanachama wa Shirikisho la Walimu Makada wa CCM kwenye Shule ya Sekondari Lugeye Wilayani Magu wakati akiongoza kampeni ya kupanda miche 400 ya miti, Mkuu huyo wa Mkoa amesema   miti ina faida nyingi katika maisha ya Binadamu hivyo kuna umuhimu wa kuitunza.

"Katika maisha ya Binadamu hana mbadala wa chakula na maji ambapo chanzo chake ni uwepo na miti, hivyo vizazi vyetu na vijavyo ni lazima vielimishwe vya kutosha kuhusu umuhimu wa miti," amesema Mkuu wa Mkoa.

Mhe. Malima amebainisha kuwa Mataifa yaliyoendelea huwezi ukasikia wamekumbwa na ukame hii ni kutokana na kuelimika vyema tangu zamani kuhusiana na thamani ya miti na misitu kwa ujumla.

"Leo naongoza kupanda miche hii 400 lakini nawahakikishia nitakuwa nafuatilia maendeleo yake nikiwa na nia ya kutaka Sekondari hii ya Lugeye iwe ya mfano wa kuigwa kwa kuwa na utitiri wa miti" amesisitiza Mhe. Malima.

Awali akimkaribisha wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe, Salum Kalli amesema maagizo yote yaliyotolewa na Mhe Malima kazi yao ni kuyatekeleza hasa wakitambua umuhimu wa miti na mazingira bora kwa mwananchi.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Walimu Makada wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Mwanza, Jackson Kadutu amesema katika kuiunga mkono Serikali ya awamu ya Sita wameamua kupanda miche hiyo pamoja na kugawa taulo za kike zenye thamani ya Shs milioni mbili na nusu kwa wanafunzi 300 na wengine 150 wenye mahitaji maalum.

"Huu ni utaratibu tuliojijengea kwa muda mrefu na mwaka huu tumefanya hivi pamoja na kukukaribisha rasmi Mkoani Mwanza Mkuu wetu wa Mkoa" amesema Kadutu.

Aidha Shirikisho hilo lenye mchanganyiko wa Walimu wa Vyuo, Sekondari na Msingi, limeshirikisha Halmashauri zote za Mwanza kwa kupanda miche 10,000.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti