RC Mongella atoa Mchango kuunga Mkono Nguvu za wananchi ujenzi wa shule ya Nkilizya
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella atoa laki tano ili kuunga mkono juhudi za wananchi katika ujenzi wa shule ya sekondari Nkilizya inayojengwa kwa nguvu za wananchi ikiwa na vyumba vinne vya madarasa na viwili vya ofisi.

Aidha amekagua ujenzi wa vyoo vya wanafunzi yenye matudu 31iliyogharimu zaidi ya million 38 ( 38,593,500.68 ) kutoka serikali kuu kupitia program ya SWASH katika shule ya msingi Namagubo hivyo Mongella alipongeza ujenzi huo kuwa unetekelezwa ipasavyo.

Kwa upande wake ofisa mtendaji wa kata ya Nansio Felister Bupamba anasema kukamilika kwa mradi huo watoto wapatao 1,576 watapata huduma hiyo kwa wastani wa watoto 79 kwa kila tundu tofauti na awali ambapo matundu 8 yalitumika .

Alisema usafi wa mazingira utaimarika,hali ya kiafya kwa watoto utaimarika na kuongoza ufaulu sambamba na hali ya wananchi kuunga mkono serikali kwenye maendeleo itaongezeka .
